Habari zinadai kuwa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich hajafurahishwa na kitendo cha Chelsea kumaliza msimu mikono mitupu bila taji lolote, na usiku wa leo anaweza kuwa tayari kutembeza kishoka kama kawaida yake baada ya fainali ya UEFA Champions.
Chanzo kimoja cha Ufaransa, Le10Sport kimedai kuwa mkataba wa Simeone unamruhusu kuondoka kama akipata mahali penye maslahi zaidi, hivyo Chelsea wanaweza kumpata kirahisi Mwargentina huyo na kumleta Stamford Bridge.
Simeone alihusishwa na tetesi za kazi ya kuinoa Manchester United kabla ya kupatikana kwa Louis van Gaal. Kocha huyo amevuta usikivu wa mashabiki wengi kwa falasafa yake ya soka aliyoipandikiza pale Atletico Madrid.
Leo jioni Atletico itashuka dimbani mjini Lisbon, Ureno katika mechi ya fainali dhidi ya Real Madrid. Maajabu kweli haijawahi kutokea katika historia ya soka Ulaya. Madrid - Madrid kukutana.
Waweza kutoa maoni yako hapo chini:
Je, Abramovich atakuwa sahihi kumtimua Jose Mourinho Chelsea?












