Jose Mourinho ameelezea mipango yake kumtumia Juan Mata msimu
huu, jambo linaloonekana kumaliza tetesi kwamba nyota huyo angeondoka Chelsea.
Muhispania
huyo aliripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wasiomvutia bosi wa Chelsea
Mourinho, pamoja na kutajwa mara kadhaa kwenye tuzo ya mchezaji bora wa klabu
wa msimu, lakini Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesisitiza kwamba Mata ana
mchango mkubwa Chelsea.
‘Hata
hivyo anafaa kwenye plan zangu,’ alisema Mourinho. ‘ Ninajua mahali pa
kumtumia, mahali anapopata ugumu ndipo anapofanya vema.
‘Tutajaribu
kumsaidia kufanya vizuri zaidi maeneo yanayomshinda. Huwa napenda sana
kuwatumia wachezaji wanaochezea mguu wa kulia kucheza kushoto.
‘Nilianza
na (Arjen) Robben na (Damien) Duff, kisha (Goran) Pandev nikiwa Inter, na
(Angel) Di Maria pamoja na (Mesut) Ozil. Kila klabu hufanya hivyo, ni nzuri.
‘Napenda
winga anaposhuka na kupenyeza kwa ajili
ya mashambulizi kwa pasi, na mashuti pia. Juan ni mchezaji pekee tuliye naye atakayefanya
hilo upande wa kulia.’
‘Upande
wa kushoto tuna (Eden) Hazard, Victor Moses, Kevin De Bruyne, Andre Schurrle.
Juan anakuwa huru sana kucheza namba 10 pia. Kati ya sehemu hizi mbili ana mengi
ya kuifanyia timu.’




0 comments:
Chapisha Maoni