KLABU ya Arsenal sasa imegeuzia mawindo
wake kwa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema katika harakati zake
za kusaka mshambuliaji mpya chaguo la kwanza.
Licha ya ukweli kwamba Real Madrid ina
washambuliaji wachache wa kati, lakini kocha Carlo Ancelotti anaweza
kumuuza mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Na klabu hiyo ya London Kaskazini imefanya mjadala mzito juu ya kumsajili mshambuliaji huyo.
Anatakiwa: Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema (kulia) anatakiwa na kocha wa Arsenal, Arsene Wenger
Kocha Arsene Wenger anamzimikia kwa muda mrefu Benzema ana amejaribu kumsajili mshambuliaji huyo mara kadhaa bila mafanikio.
Lakini Arsenal sasa wanaonekana kuwa
katika nafasi nzuri ya kumnasa mshambuliaji huyo kabla ya kufungwa kwa
pazia la usajili Septemba 2.
Wenger amepagawa mno baada ya kuwakosa
washambuliaji aliokuwa anawataka Luis Suarez na Wayne Rooney, lakini
wakimpata Benzema watapunguza matatizo.

Anafunga: Benzema aliifungia Madrid dhidi ya Real Betis katika mchezo wa ufunguzi wa La Liga

Wamemkosa: Luis Suarez hatajiunga na Arsenal majira haya ya joto




0 comments:
Chapisha Maoni