Alikuwa mshabiki wa kutupwa wa Yanga na CCM
![]() |
| Askofu Mosses Kulola enzi za uhai wake |
Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk.Moses Kulola amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Taarifa za kifo cha askofu huyu maarufu aliyekuwa mshabiki wa kutupwa wa timu ya Yanga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimetolewa na mtoto wake Mwinjilisti Daniel Kulola kupitia mtandao wa “face book”ambapo ameueleza umma wa watanzania kuwa baba yake mzazi amefariki dunia katika hospitali ya Ami iliyoko Msasani, jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.
Hajaeleza marehemu alikua anaumwa nini lakini taarifa zinasema amekuwa mgonjwa siku nyingi ambapo aliwahi kulazwa nje ya nchi na baadae akarudishwa nchini na hatimae kufariki Dunia.
Hadi hivi sasa haijajulikana askofu Kulola atazikwa lini lakini pia taarifa zimethibitishwa rasmi kutoka kwa wachungaji mbalimbali ambao wako chini ya kanisa lake ambalo lina mtandao nchi nzima na lenye waumini zaidi ya milioni 5 nchini kote.
Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.
Alimwoa Elizabeth na wamezaa watoto10 ambapo saba bado hai.alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa.
Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.
Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.
Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzisha kanisa la Evangelistic Assemblies God (EAGT) baada ya kutokea mvutano ndani ya kanisa la TAG, ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.
Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe

| Askofu Kulola enzi za ujana wake |

bora fitina ipungue yanga majungu fitna R.I.P kulola jana yanga droo huo ndio mpira
JibuFuta