The reliable source of sport news

Jumanne, Agosti 27, 2013

Mourinho amempa Rooney masaa 48 kuamua mustakabali wake

27.8.13 By Unknown No comments

MANCHESTER // Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, amemwambia Wayne Rooney kufanya uamuzi ndani ya siku mbili kama anataka kuhamia Chelsea ama kubaki Manchester United.

"Anayeanza stori ndiye mmalizaji wa stori," Mourinho alisema Jumatatu baada ya sare ya 0-0 ya Chelsea dhidi ya Manchester United mchezo ambao Rooney alikuwepo.
Rooney aliashiria kuwa anataka kuondoka mwishoni mwa msimu uliopita, na mabingwa wa ligi ya Uingereza walizitosa ofa mbili za Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji huyo. Kauli kuu ya Manchester kipindi chote cha majira ya joto, ni Rooney hauzwi.

"Iwapo sasa hataki kuondoka Old Trafford, basi tutakuwa tumeshindwa sisi," alisema Mourinho, "lakini tunataka kujua nini kinaendelea."
"Tutasajili mchezaji mwingine kama hayuko tayari kujiunga nasi," aliongeza Mourinho, ambaye amehusishwa mshambuliaji wa Anzhi Makhachkala, Samuel Eto'o.
Alipoulizwa: Je unataka Rooney aje kutoa tamko kuhusu uamuzi wake , Mourinho alisema: "NDIYO," na kuongezea kuwa anataka jibu ndani ya masaa "24, na 48."
Rooneyalicheza dakika zote katika mechi dhidi ya Chelsea. 
Mourinho alisema Rooney amecheza kama "mchezaji wa kimataifa" na ilipendeza sana.

0 comments:

Chapisha Maoni