Barcelona imethibitisha kwamba Mwajentina
Gerardo Martino ndiye kocha mteule wa timu hiyo kufuatia kujiuzulu kwa Tito
Vilanova kwa sababu za kiafya.
Kutoka kwenye tovuti ya Barca, mabingwa hao wa Hispania wamesema:
"Gerardo Martino, kocha mpya FC
Barcelona. FC Barcelona imefikia makubaliano kumsajili Gerardo Martion kama meneja wa kwanza wa klabu hiyo kwa misimu miwili ijayo."
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia ni meneja wa zamani wa Newell's Old boys atakuwa Mwargentina wa nne kushika wadhifa huo katika historia ya klabu ya Catalans kufuatia Roque Olsen, Helenio Herrera na Cesar Luis Menotti.
"Sikuwa nimetarajia hili, Nilikuwa
nikijiandaa kupumzika mara nilipopokea simu toka Barca, najivunia kupata fursa
hii." Martino aliiambia tovuti ya Barcelona. "Nina furahi sana
Barcelona kunifikiria kwa kazi hii njema"
Martino atakuwa na muda mchache wa kujiandaa kitu ambacho kitakuwa
ni mtihani katika kazi yake ya ukocha – kuiongoza Barcelona kutetea taji lake
la La Liga, kurejesha hadhi ya Nou Camp katika ligi ya klabu Bingwa (Baada ya
kipigo cha mbwa mwizi cha 0-7 toka kwa
Bayern Munich) na kuwashinda mahasimu wao Real Madrid wanaoongozwa na Carlo
Ancelotti.
Barcelona ina ratiba ya kucheza mchezo wa kirafiki na Bayern
Munich Jumatano: Mechi hiyo ni sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa nyota wa kimataifa Thiago
Alcantara kwenda mabingwa hao wa Bundesliga na Ulaya pia.
Pia inaeleweka kwamba Martino hatakuwepo benchi kwenye mechi hiyo
ya kirafiki baina ya Barcelona na Bayern Munich, ingawa anaweza kuanza kwenye
mechi ya kirafiki itakayopigwa kati ya Barca na Valarenga ya Norwei
itakayochezwa Ijumaa.
Kocha mpya huyo wa Barcelona atakuwa na wakati mgumu kufanya
maamuzi kwamba amruhusu Cesc Fabregas kwenda Manchester United ama la.
Muhispania huyo amehusishwa na ofa mbili ambazo hazikufanikiwa za
Manchester United kutaka kumnunua, ofa ya mwisho ilikuwa pauni milioni 30.
Kufuatia hili inaaminiwa kwamba Barcelona imeachia maamuzi hayo kwa kocha mpya,
ambaye kwa sasa amepatikana Martino.
Ingawa
bado kuna sababu zitakazomfanya Moyes aendelee kufadhaika, Kuna sababu kuu
mbili za msingi.
Ya kwanza
ni: Martino anaamini sana kuchezesha viungo zaidi na atamfikiria kucheza na
viungo wenzake wa Hispania kama Andres Iniesta na Xavi Hernandes, kupitia
gazeti mojawapo la mwaka jana Martino alisikika akisema “Aina ya uchezaji wa
Barcelona haitabadilika, lakini itakuwa ni vigumu sana kudumisha mchezo huo
bila ya wachezaji mahiri kama Iniesta, Xavi na Cesc”. Inaeleweka kwamba kocha huyo mpya wa Katalans
atakuwa na shauku ya kuendeleza huduma ya Fabregas klabuni hapo.
Sababu ya
pili ni kuondoka kwa kiungo mwingine wa kihispania – Thiago Alcantara. Nyota
huyo naye Manchester United ilimtafuta sana lakini juhudi za Moyes
hazikufanikiwa kiungo huyo alipofikia hatua ya kuitosa Manchester United na
kutimkia Bayern Munich jambo lililomfanya Moyes kumgeukia Fabregas.
Inaonekana
Fabregas atabakia Nou Camp, angalau kwa msimu huu, na Moyes atalazimika kuangaza
macho kwengine kuboresha nafasi yake ya kiungo.





0 comments:
Chapisha Maoni