The reliable source of sport news

Jumatano, Julai 24, 2013

Majeraha ya Robin Van Persie yaitoa Manchester United Jasho

24.7.13 By Unknown No comments

Robin Van Persie alitolewa wakati Manchester United ilipopokea kipigo cha mabao 3 kwa 2 toka kwa Yokohama F-Marinos Jumanne.

David Moyes ana hofu zaidi ya kipigo mechi hiyo ya maandalizi ya kuanza msimu, mshambuliaji wake Van Persie alitolewa nje baada ya
kupata majeraha kwenye paja. Ilikuwa chungu kwa meneja huyo mpya kushuhudia timu yake ikipoteza mechi ya pili kati ya tatu walizocheza.

Kabla haijatangazwa ni kiasi gani nyota huyo amejeruhiwa, Moyes aliamua kufanya mabadiliko mara alipomwona mchezaji huyo akishika paja na kupata matatizo kutembea. Kwa sasa anasubiri ripoti ya daktari kwamba ni kiasi gani nyota huyo ameumia.

Pamoja na majeraha ya Van Persie, David Moyes amepokea habari njema kwamba Wayne Rooney aliyekuwa amepata majeraha siku kadhaa zilizopita atakuwa fiti siku chache zijazo na ana imani ataweza kurudi uwanjani hivi karibuni.

Wakati akihojiwa, David Moyes alisema, Van Persie alishindwa kuendelea na mchezo kwasababu ya majeraha, vilevile Welbeck naye bado ana majeraha.

"Tumepata hofu kwa kweli" Moyes alimwambia Ripota, "Van Persie amepata majeraha pajani kipindi cha kwanza na hakuweza kuendelea, Danny Welbeck naye pia ni majeruhi na tunaloweza kufanya ni kuhakikisha wanakuwa sawa hasa kwa michezo inayofuata." Alisema bado wana michezo michache imebaki kabla ya kurudi kuanza msimu.

Alipoulizwa kuhusu Wayne Rooney, alisisitiza kwamba Rooney hauzwi.

0 comments:

Chapisha Maoni