The reliable source of sport news

Jumatatu, Julai 22, 2013

Nagoya Grampus 1 Arsenal 3: Ushindi mlaini kwa The Gunners dhidi ya timu ya Wenger ya zamani

22.7.13 By Unknown No comments

Angalau mambo yanakwenda kama yalivyopangwa kwa upande wa Arsenal katika maandalizi ya kuanza msimu wa majira ya joto. Wakati klabu inapong’ara na kuziba mapengo kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa kama walivyoahidi mashabiki. The Gunners wamefunga goli lao la 17 katika mechi tatu za kujiandaa kuanza msimu wa ligi leo huko Japan, kwa ushawishi wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya zamani ya Nagoya Grampus.


Olivier Giroud ameendeleza makali yake kwa kuipatia magoli sita Klabu yake kwenye ziara hiyo ya mashariki ya mbali, alifunga bao la kwanza kasha mchezaji wa kimataifa wa Japan Ryo Miyaichi na Theo Walcott kufunga goli moja moja na kukamilisha ushindi wao wa mabao matatu kwa moja.

Ulikuwa ni mchezo wa aina yake uliowapa wachezaji wa Arsenal morali baada ya kupata ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya timu ya Indonesia Dream Team na ushindi mwingine wa mabao 7-1 dhidi ya Vietnam XI. Wenger aliyeondoka Nagoya Grampus kujiunga na Arsenal mwaka 1996 alipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Japan wanaomkumbuka bado kwa kazi yake njema wakati akielekea kusalimiana na mchezaji wake wa zamani ambaye ni kocha wa timu hiyo kwa sasa Dragan Stojkovic.


Bosi wa The Gunners alishuhudia timu yake ikianza kufunga bao la kwanza dakika ya tatu toka kwa Giroud, nyota huyo alifunga goli safi kwa kichwa.

Chumba cha Arsenal cha kubadilishia nguo kama kinavyoonekana kabla ya mechi kuanza
Wenger aliondoka kwenye uwanja wa Toyota akiwa na matumaini makubwa baada ya kuona kandanda safi aliloonyesha Bacary Sagna, Wenger ana hofu na nafasi za Thomas Varmaele na Laurent Koscielny ambao wote hawapo kutokana na majeraha.

0 comments:

Chapisha Maoni