The reliable source of sport news

Jumatano, Julai 31, 2013

Mtaka vyote hukosa vyote, Eti Arsenal inamtaka Luka Modric Sasa

31.7.13 By Unknown No comments

Arsene Wenger amekuwa akimbwela mbwela kipindi chote cha usajili wa majira ya joto, alitaka kumsajili Higuain akazubaa hadi akanyakuliwa na Napoli, Marouane Fellaini naye hakijaeleweka hadi leo aliambulia YAYA SANOGO tena kwa uhamisho huru. Amejaribu kupeleka ofa kwa ajili ya Luis Suarez, maji yamekuwa marefu zaidi, Sasa kwa Modric, Je kuna asubuhi hapa?. TAFADHALI KOMENTI HAPA CHINI MAONI YAKO.


Manchester United na Arsenal zinajipanga kufanya mchakato wa kumnyakua nyota wa Real Madrid Luka Modric baada ya Arsene Wenger naye kujiunga katika mbio hizoare set to go head-to-head over Real Madrid star Luka Modric after Arsene Wenger joined the race for the Croatian international, Kwa mujibu wa Daily Star.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 hana uhakika wa kupata namba Bernabeu baada ya kufanya vibaya msimu uliopita kwenye ligi ya Hispani La Liga. 
Manchester United imekuwa ikimtamani Modric kwa muda mrefu, lakini inasemekana kwamba Arsenal nayo imemgeukia kiungo huyo wa Real Madrid baada ya kuwakosa mastaa wote iliyolenga kuwasajili.
The Gunners walimkosa Gonzalo Higuain ambaye alitimkia Napoli na wana ofa kadhaa zilizokataliwa na Liverpool kwa ajili ya Luis Suarez.
Hata Mbrazil Bernard anaonesha mwelekeo wa kujiunga na Porto au Shakhtar Donetsk badala ya Arsenal.
Nia ya Manchester United kupata Kiungo wa kati ni njema ingawa hadi sasa hawajapata, na jitihada zao za kumleta Fabregas zimegonga mwamba.
Thiago Alcantara ilikuwa nusura ajiunge na Manchester United lakini Bayern Munich ikatibua mambo na kuinyang’anya Man U tonge mdomoni..

Na ripoti zinasema Arsenal and Manchester United ziko kwa Luka Modric, mchezaji anayeweza kuwa na wakati mgumu Bernabeu kufuatia usajili wa Isco na Asier Illarramendi.

0 comments:

Chapisha Maoni