Tangu uhamisho wa pauni
milioni 15 kwenda Barcelona, Kipaji cha Song uwanjani kimekuwa hakitambuliki
kwa walio wengi sasa.
Je, ni sawa Song
kufikiria kurudi Arsenal tena?
Song,
25, amecheza michezo isiyopungua 38 kwa msimu akiwa Arsenal misimu minne
iliyopita alipokuwa Arsenal na akatambulika kwa ustadi wa kazi yake nafasi ya
kiungo na kwa upande mwingine kiungo mkabaji.
Alithaminiwa sana katika msimu wake wa mwisho Arsenal, ambapo
alicheza mechi 46 akifunga goli moja na kutoa pasi 14 za magoli.
Hakika
anakumbukwa katika msimu huu kwa ushirikiano wake na Robin Van Persie
uliowafanya mabeki wengi kushindwa kuizuia Arsenal.
Tangu
aondoke umepita mwaka sasa, Song amepata fursa ya kuichezea Barcelona mara 20
tu, hajafunga goli hata moja na amefanikiwa kutoa pasi moja ya goli kwa miamba
hao wa Catalan.
Hajaweza
kuwashawishi mashabiki wa Barcelona, ushawishi wake umekuwa mdogo sana.
Ingawa
Arsenal imekuwa klabu inayouza wachezaji miaka ya karibuni, lakini mwaka huu
imeshindwa kufanya hivyo.
Sasa
wanahitaji kununua wachezaji wakubwa na Luis Suarez akiwa moto moto midomoni
mwa mashabiki wa Arsenal na kwa nia njema Arsenal imepeleka ofa kadhaa kwa
ajili ya nyota huyo raia wa Uruguay.
Lakini
uchaguzi mrahisi kwa Arsenal utakuwa Alex Song. Mchezaji aliyethaminiwa na Arsenal
na ameichezea michezo mingi lakini hapewi nafasi Barcelona.
Kwa
kiwango cha fedha walicho nacho Arsenal itakuwa rahisi kwao kuboresha kikosi
chao kwa kumrejesha nyota huyo Arsenal.
MAONI YAKO NI YA MUHIMU SANA
MAONI YAKO NI YA MUHIMU SANA




0 comments:
Chapisha Maoni