The reliable source of sport news

Jumapili, Agosti 04, 2013

Meneja wa Chelsea amwongelea Fernando Torres, Anasemaje? Soma hapa ujionee

4.8.13 By Unknown No comments

Wakati habari za Wayne Rooney kuhamia Chelsea zikitawala habari nyingi za Chelsea katika dirisha la uhamisho tangu ujio Jose Mourinho, haiwezi kusahaulika kwamba Fernando Torres bado yumo klabuni hapo.

Straika huyo alifurahia kipindi cha mwisho cha msimu akiwa na kocha wa muda Chelsea, ingawa kiwango chake akijalingana na kiasi cha fedha zilizolipwa wakati wa uhamisho wake.


Sasa chini ya meneja mpya Mourinho, Torres amepewa fursa nyingine kumshawishi kocha huyo kupata namba katika kikosi chake cha kwanza. Itakuwa si kazi rahisi kwake kwasababu The Blues inamwajiri Romelu Lukaku na Demba Ba wote katika nafasi moja. Kwa upande mwingine, endapo Chelsea itafanikiwa kukamilisha uhamisho wa Wayne Rooney italeta changamoto na upinzani wa hali ya juu katika klabu hiyo ya Stanford Bridge. 
"Sijui kama ni kujiamini. Nahisi anajituma na ni mchapa kaziI," Mourinho alikiambia chanzo cha Sky Sports
"Nadhani shughuli zote za timu zinazohusiana na mashambulizi zinaendana na ubora wake. Tupo hapa kwa ajili ya kumwezesha.

"Tunapomwona Torres akiwa na beki golini huku amezungukwa na maadau kama wawili ama watatu tunajia kwamba hawezi kufanya muujiza.

"Hatuhitaji timu ijifunze namna ya kucheza naye lakini kuboresha namna ya kucheza naye. Anajitahidi sana kwenye mazoezi na tunamfurahia.
"Si rahisi kurekebisha jinsi anavyocheza tena. Lakini tunataka kuifunza timu jinsi gani ya kutumia uwezo wake.

"Si mtoto tena. Yuko katika umri ambao ni vigumu kubadili staili yake ya mchezo. Atabaki kama alivyo na ana uwezo mzuri hivyo tunahitaji  kujifunza na kumwezesha."
Haijalishi kama Rooney anakuja Chelsea ama haji, itajulikana atakapokuja, lakini Torres atapaswa kufikiria sana mustakabali wake. Na wakati kombe la dunia likikaribia Torres anapaswa kuhakikisha kwamba anaichezea klabu yake mara kwa mara.

0 comments:

Chapisha Maoni