David Moyes, ambaye sasa ni Meneja wa
Manchester United, akiri kwamba alilala kwenye gari wakati wa kombe la dunia
lililofanyika Ufaransa mwaka 1998.
Kipindi hicho, wakati akianza kujifunza
shughuli za umeneja wa mpira wa miguu, Moyes alianza kutafuta namna mbalimbali
za kuvumbua wachezaji wenye vipaji sehemu tofauti tofauti duniani. Mscotish huyo amekiri kwamba mara nyingine ilimbidi alale kwenye
gari wakati wa ziara yake hiyo.
Akiongea na watangazaji, Moyes said: "Kipindi
cha kombe la Dunia kule Ufaransa mwaka 1998, Ndiyo tu nilikuwa nimeteuliwa kuwa
meneja wa Preston. Nilikiomba chama cha wataalamu wa mpira kuniwezesha kifedha
iIi niende kwenye kombe la dunia kwa mafunzo.
"Niliziandikia
nchi nyingi kuona kama nigepata fursa ya kwenda kutazama mafunzo.
"Aliyenijibu
alikuwa Craig Brown wa Scotland – na mimi pia nilikuwa mscottish.
"Nilipata
tiketi kutazama baadhi ya michezo, lakini hazikutosha. Lakini nilikodi gari
dogo. Nilipewa fedha na PFA. Sikuwa nikipata fedha za kutosha.
"Mwishoni
ilinilazimu kuendesha na ilinibidi kulala kwenye gari mara kadhaa. Hilo ndilo
nililofanya kuongeza ujuzi zaidi."
Maisha
ni tofauti sasa kwa bosi huyo wa Mashetani wekundu – Moyes amerudi toka ziarani
ambako alizitembelea Japan, Thailand, Australia na Hong Kong.
Na
ndani ya kipindi cha wiki mbili, Agosti 11, kocha huyo mwenye umri wa miaka 50
atakuwa na kibarua cha kuiongoza timu yake uwanja wa Wembley dhidi ya Wigan
Athletic mechi ya ngao ya Hisani.
Toka
kulala kwenye gari hadi Old Trafford – imekuwa ni safari kwa David Moyes.




0 comments:
Chapisha Maoni