![]() |
| Wamemkosa tena: Wesley Sneijder akiwa mazoezini na Uholanzi nchini Katwijk leo |
United awali ilikaribia kumsajili kiungo
huyo Mholanzi kutoka Inter Milan mwaka 2011 kwa dau la Pauni Milioni
35, lakini iliamua kuachana na Sneijder baada ya kutaka mshahara wa
Pauni 200,000 kwa wiki.
Pamoja na hayo, sasa inasemekana United
ilifufua mpango wa kumsajili mchezaji huyo chini ya kocha wake mpya,
David Moyes, huku Galatasaray ikisema klabu hiyo ya Old Trafford
ilimgeukia Sneijder baada ya kukwama kuwasajili Cesc Fabregas na Thiago
Alcanatara mapema majira haya ya joto.

Anabaki: Wesley Sneijder yuko mazoezini na kikosi cha Uholanzi nchini Katwijk leo

Mholanzi kiwango: Kocha wa Uholanzi, Louis van Gaal anakiandaa kikosi chake kwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia wiki hii
Mratibu wa Michezom, Bulunt Tulun
ameliambia gazeti la Uturuki, Milliyet kwamba: "Sneijder amepokea ofa
kutoka Manchester United wiki mbili zilizopita, lakini haikukubaliwa.
Kulikuwa kuna klabu kadhaa zinamtaka, lakini kama ambavyo hatuwezi
kumruhusu kuondoka Burak (Yilmaz) pia tunatakiwa kumbakiza
Sneijder,"alisema.
Roma ilithibitisha United ilitoa ofa ya
wazi kwa ajili ya Daniele De Rossi ya Pauni Milioni 12, ambayo ilipigwa
chini pia, wakati Mktendaji Mkuu, Ed Woodward aliripotiwa kujaribu
kumsajili kwa Pauni Milioni 30.5 kiungo wa Athletic Bilbao, Ander
Herrera.

Imedunda: United imemkosa pia Sami Khedira (juu), Daniele De Rossi (chini) na Ander Herrera (chini kabisa)


United pia ilikwama kumsajili mwanasoka
wa kimataifa wa Ujerumani, Sami Khedira ahamie Old Trafford kutoka Real
Madrid, na kiungo huyo amethibitisha mwenyewe alivyokoswakoswa na kocha
David Moyes dakika za mwishoni.
United imefanikiwa tu kumsajili kiungo
Mbelgiji wa Everton, Marouane Fellaini kwa Pauni Milioni 27.5,
anayekwenda kuungana na kocha wake wa zamani Toffees, David Moyes Old
Trafford.




0 comments:
Chapisha Maoni