BAADA ya kumsajili Mesut Ozil kwa dau la
Pauni Milioni 42.5 katika siku ya mwisho ya kufungwa kwa pazia jana,
Arsenal imepata pigo kufuatia kuambiwa Lukas Podolski anatakiwa kuwa nje
kwa miezi mitatu kwa sababu ya majeruhi.
Dawati la Madaktari la Arsenal tayari
lilikubali kumkosa mshambuliaji huyo kwa wiki kati ya nane na 10, lakini
madaktari wenzao wa timu ya taifa ya Ujerumani, walifanya uchunguzi wa
kina na kusema Podolski ana muda mrefu wa kuwa nje.
Dk Hans-Muller Wohlfahrt, ambaye
alishughulikia vipimo vya afya vya Ozil kwa niaba ya Arsenal kiungo huyo
akiwa Ujerumani kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya kufuzu Kombe la
Dunia dhidi ya Austria Ijumaa, alituma taarifa hizo Gunners leo.


Pigo: Podolski anatakiwa kuwa nje kwa miezi mitatu kutokana na maumivu ya nyama
Muller-Wohlfahrt alimfanyia vipimo
Podolski mjini Munich na kugundua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28
amechanika nyama katika mguu wake wa kushoto na atakuwa nje hadi
Desemba.
Podolski ameliambia gazeti la kila siku
la Ujerumani, Bild: kwamba "Kwa bahati mbaya nitakuwa nje kwa muda mrefu
kiasi cha miezi mitatu,".

Munja rekodi: Mesut Ozil amewasili kutoka Real Madrid kwa dau la Pauni Milioni 42.5
Podolski alitolewa nje ya kikosi cha
timu yake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Fenerbahce wiki
iliyopita. Na licha ya kusajiliwa kwa Ozil, majeruhi ya Podolski ni
poigo kwa Wenger ambaye amekwishakamilisha kikosini.
Olivier Giroud na Theo Walcott ndio
washambuliaji pekee wa kati waliobaki kwenye kikosi cha Wenger, na
mchezaji mpya Yaya Sanogo ndiye anakuwa wa akiba pekee.

Mawili: Podolski hivi karibuni ameifungia Arsenal mabao mawili katika mchezo dhidi ya Fulham Ligi Kuu ya England



0 comments:
Chapisha Maoni