MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amezalisha
hofu Manchester United baada ya kuumia kichwa jana asubuhi na sasa kuna
wasiwasi akaukosa mchezo wa leo dhidi ya Liverpool.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa England
aliumia kichwa mazoezini asubuhi na aliondoka Uwanja wa mazoezi wa timu
hiyo, Carrington HQ akiwa amefungwa bandeji iliyozunguka kichwa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 yuko shakani sasa kucheza Anfield leo na hatima yake itaamuliwa na madaktari wa timu hiyo.
Rooney alicheza soka ya nguvu United ikimenyana na Chelsea Jumatatu na kuondoa shaka juu ya mustakabali wake Old Trafford.

Kichwa kinamuuma: Kocha David Moyes amepata pigo kwa Rooney kuumia kichwa
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Chelsea,
Jose Mourinho alimtaka mshambuliaji huyo kuweka wazi ndani ya saa 48
kama anabaki au anataka kuondoka, lakini Rooney alijibu kwa kuweka
ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook amefurahishwa na mapokezi
aliyopewa na mashabiki katika mchezo huo.

Kipenzi cha mashabiki: Rooney amefurahia mapokezi ya mashabiki Old Trafford katika mechi na Chelsea
Sasa mkonwe Ryan Giggs anaweza kuchukua
nafasi ya Rooney katika mchezo wa leo, akicheza sambamba na Danny
Welbeck na Robin van Persie katika safu ya ushambuliaji. Mchezaji
anayetakiwa na Tottenham, Javier Hernandez pia amekuwa akifanya mazoezi.




0 comments:
Chapisha Maoni