The reliable source of sport news

Ijumaa, Agosti 30, 2013

MPINZANI WA CHEKA ATISHA KWA NGUMI YENYE MANUNDU

30.8.13 By Unknown No comments

Pamoja na Phill Williams kuonyesha kifua chake kilichojengeka vizuri kimazoezi kama kitisho kwa Francis Cheka, ngumi yake yenye manundu pia imeonyesha kuwashangaza wengi.

Mmarekani huyo amekuwa akionyesha mara kwa mara mkono wake ambao unafanana utafikiri amekuwa akipiga ukuta.

Lakini Cheka ambaye ameondoka muda mchache uliopita kutoka katika hoteli ya Atriums Sinza Afrika Sana kwenda Diamond Jubilee, amesema wala hana hofu.

“Najiamini, najua pambano litakuwa gumu lakini nitapambana,” alisema.
Mara kadhaa, Phills amekuwa akionyesha mkono huo kama kitisho kwa Cheka.

0 comments:

Chapisha Maoni