The reliable source of sport news

Ijumaa, Agosti 30, 2013

Messi aliogopa kundi lake UEFA Champions League

30.8.13 By Unknown No comments

Straika wa Barcelona Lionel Messi, amesema baada ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kuwa, kundi lao linaloundwa na AC Milan, Ajax na Celtic ni kundi gumu ingawa Barca inazifahamu timu zote vema.


 “Hakunaga kundi rahisi kwenye Ligi ya Mabingwa. Tunawajua Milan vema, Celtic tulicheza nao msimu uliopita. Ajax ni timu yenye historia ndefu katika soka la Ulaya,” alisema Mwargentina huyo.

“Daima kuna timu ngumu mara zote”. Timu zimepangwa vema na zinaendana, hakika kutakuwa na mechi nzuri za kusisimua kwa mashabiki. “Timu za kundi letu zinafahamiana vizuri na kundi letu ni gumu sana,” aliendelea kusema kwenye mjadala wa Grimaldi katika Monaco.
Messi pia aliizungumzia miamba ya Catalan kuhusu msimu uliopita “Michuano ya msimu uliopita iliisha vizuri” kwasababu mwisho wa yote Barcelona ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Hispania na kuiachia manyoya Real Madrid.

“Tulishinda ubingwa mkuu mwaka jana. Lakini tulipoteza ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya kwa Bayern Munich, waliokuwa bora zaidi yetu. Tuna matumaini ya kushinda mataji mwaka huu,” Aliongeza nyota huyo.


“Malengo yetu ni kushinda kila taji klabu yetu inalostahili kushinda. Tunajua kuwa kila mwaka michuano inakuwa migumu kwasababu kila timu inaleta wachezaji wapya kuimarisha safu zao ili kuweza kushindana, lakini tumejiandaa kwa hilo pia.” alihitimisha.

0 comments:

Chapisha Maoni