The reliable source of sport news

Jumatatu, Agosti 05, 2013

Cristiano Ronaldo asaini mkataba mpya wa miaka mitano wenye thamani ya pauni milioni 75 Real Madrid

5.8.13 By Unknown No comments

Imeripotiwa kwamba Cristiano Ronaldo amesaini mkataba wa miaka mitano na Real Madrid wenye thamani ya pauni milioni 75. Mkataba huo utamfunga klabuni hapa kipindi chote kilichobaki cha soka lake. 
Mreno huyo amekuwa akihusishwa mara kadhaa na tetesi za kurudi Manchester United lakini amefikia uamuzi wa kubaiki na miamba hao wa La Liga.


Gazeti linalomilikiwa na Madrid - Marca limeripoti kwamba Ronaldo atakuwa akilipwa kiasi cha £900,000 zaidi kila msimu zaidi ya Supastaa wa Barcelona Lionel Messi, jambo litakalomfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi kuliko wote katika Ligi ya Hispania.
Ronaldo, aliyeigharimu Madrid £80millioni mwaka 2009, alikutana na rais wa klabu Florentino Perez huko Los Angeles wakamaliza tofauti zao.

0 comments:

Chapisha Maoni