Miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uvumi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Hispania na Uingereza kwamba Jose Mourinho anataka kumuuza beki mbrazili David Luiz.
Fununu zimesikika kwamba Luiz alikuwa tayari kuondoka Chelsea kujiunga na Barcelona kwa kukubali makato kwenye malipo yake.
Lakini, El Mundo Deportivo kimeripoti Jumatano hii asubuhi kwamba Jose Mourinho hayuko tayari kuiruhusu Barcelona kumchukua beki huyo wa Chelsea.
Wakati huo gazeti la The Sun nalo limeripoti kwamba Barcelona inakaribia kumsajili nyota huyo beki wa Chelsea.
Imeripotiwa kwamba Jose Mourinho amebadili msimamo wake huo kuhusu David Luiz wa miezi kadhaa iliyopita kwamba Luiz yupo tu kwasababu ya msimamo na hadhi ya Chelsea.
Mmiliki wa Roman Abramovich anayedaiwa kuwa shabiki namba moja wa Luiz na Mourinho wanaamini kwamba wanaweza kuimarisha uwezo wa beki huyo aliyejiunga na klabu hiyo akitokea Benfica.
Barcelona sasa inaangalia uwezekano wa kuipata huduma ya beki wa Liverpool Daniel Agger na inaaminika kwamba Barcelona wanaweza kukata tamaa ya kupata beki mpya na hivyo kurudisha imani yao kwa beki wa kati mkongwe Carles Puyol ambaye anarudi baada ya kupona majeraha.




0 comments:
Chapisha Maoni