![]() |
| Picha ya Wayne Rooney ikionyesha jinsi alivyoumia kichwani |
Straika
wa Uingereza, Wayne Rooney amepost picha mtandaoni picha inayoonyesha jinsi
alivyojeruhiwa kichwani, majeraha yaliyomfanya akose mechi za kuwania kufuzu
kombe la Dunia.
Nyota
huyo mwenye umri wa miaka 27, alikosa mechi ya Manchester United wakati ilipocheza
dhidi ya Liverpool (Waliyokula kichapo cha 1-0) Jumapili iliyopita baada ya
David Moyes kuthibitisha kuwa amepata majeraha kichwani kufuatia kugongana kwa
bahati mbaya na mchezaji mwenzake Phil Jones walipokuwa kwenye mazoezi.
Moyes
alieleza kuwa ana imani Rooney atapona mapema na kujiunga na wenzake kwenye
timu ya Taifa itakayocheza dhidi ya Moldova na Ukraine.
Rooney
ameweka picha inayoonyesha majeraha yake kwenye ukurasa wake wa facebook
Jumatano jioni ikifuatiwa na maelezo machache kama yanavyoonekana kwenye ayah
ii hapa chini.
"Baadhi
ya watu wanajiuliza kama nitaitumikia Uingereza kipindi hiki ama la, ki ukweli
nimeamua kujito kwenye michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia," aliandika.
![]() |
| Ukurasa wa Facebook wa Wayne Rooney ukionyesha jinsi alivyoandika kuhusu majeraha yake ya kichwani |
"Hakuna
shaka, napenda kuwa pamoja na wenzangu kuwania kufuzu kucheza kombe la Dunia. Nina
imani watu wakiona picha hii wataelewa ni kwanini siwezi kucheza kipindi hiki."
Mchezaji
mwenzake Theo Walcott alieleza jana kuhusu kidonda hicho "kinafanana na
majeraha ya kwenye filamu za kutisha".
Uingereza
itaumana na Moldova na Ukraine, kwa sasa iko nyuma ya vinara Montenegro kwa
point 2 lakini ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
Rooney,
ambaye alihusishwa sana na uhamisho kwenda Chelsea kabla dirisha la usajili
halijafungwa, aliamua kubaki Manchester United.
Lakini
majeraha hayo yanamaanisha Rooney, aliyeichezea England mara 84 na kufunga
magoli 36, atakosa mechi kadhaa za kuwania kufuzu kombe la dunia wakati
wachezaji wenzake Danny Welbeck, na nyota wa Liverpool Daniel Sturridge
watakaposhuka dimbani.





0 comments:
Chapisha Maoni