The reliable source of sport news

Alhamisi, Septemba 05, 2013

USAJILI LIGI YA MABINGWA ULAYA HUU HAPA...MOURINHO AMTEMA ESSIEN CHELSEA

5.9.13 By Kapoma No comments

Nje Ulaya: Michael Essien (kushoto) amekuwa akiishia kusugua benchi mechi tatu za Chelsea mwanzoni mwa msimu na ametemwa kikosi cha Ulaya
VIUNGO Michael Essien na Darren Fletcher ndio majina makubwa ya wachezaji waliotemwa katika vikosi vya wachezaji 25 wa klabu zao kwa ajili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Essien alikuwa kwa mkopo Real Madrid msimu uliopita na amerejea Stamford Bridge chini ya kocha Jose Mourinho. 
Lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa akiishia kusugua benchi katika mechi zote tatu kati ya nne za ufunguzi za The Blues msimu huu na hatacheza michuano ya Ulaya. 

Nahodha wa Scotland, Fletcher amecheza mechi 13 tu tangu alazimike kusimama soka kwa maradhi mwaka 2011. 
Uamuzi wa David Moyes kumtema Fletcher katika kikosi cha United unatokana na kuhofia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hataweza kurejea kwenye kikosi cha kwanza mwaka huu na wakati hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa inamalizika Desemba.
Agosti, Fletcher alijizuia kufika kwenye Uwanja wa mazoezi wa United, AON Complex mjini Carrington.
Missing: Darren Fletcher 
hasn't played since December
Nje: Darren Fletcher hajacheza soka tangu Desemba

"Bado niko mbali na viwanja vya mazoezi hadi sasa, tu kwa sababu ni vigumu kwenda huko wakati hufanyi mazoezi. Nimezungumza na kocha, anaonekana poa na tumejadili mipango ya mbele,"alisema mchezaji huyo ambaye ameongeza akiwa fiti ataanza mazoezi mara moja. 
Staying away: Fletcher 
revealed he isn't going to Carrington but remains positive
Bado yuko mbali: Fletcher amesema haendi Carrington kwa sababu hafanyi mazoezi
Loan move: Adnan Januzaj isn't
 in Man United's 25-man squad and could play elsewhere this season
Wa mkopo: Adnan Januzaj hayuko kwenye orodha ya wachezaji 25 wa Man United wa Ulaya

Wakati huo huo, kinda mwenye kipaji, Adnan Januzaj, ambaye alikwenda kwenye ziara ya klabu ya kujiandaa na msimu Mashariki ya Mbali na Australia na kufanya vizuri pia ametemwa kwenye kikosi hicho.
Inafahamika Mbelgiji, ambaye atapewa Mkataba mpya wa miaka mitano katika klabu hiyo, anaweza kutolewa kwa mkopo.
Pamoja na hayo, makinda wenzake Sam Johnstone, Jesse Lingard, Tom Thorpe, Will Keane na Larnell Cole wameorodheshwa katika kikosi cha pili, Man United B.
Wachezaji wapya Wilfried Zaha na Marouane Fellaini wamo kwenye kikosi hicho. 

VIKOSI VYA TIMU ZA UINGEREZA KATIKA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA MSIMU HUU NI HIVI...

Arsenal: Szczęsny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Koscielny, Rosický, Arteta, Podolski, Wilshere, Özil, Giroud, Viviano, Walcott, Oxlade-Chamberlain, Ramsey, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabiański, Sanogo, Jenkinson, Gibbs, Ryo, Bendtner. Zelalem
Chelsea: Cech, Schwarzer, Ivanovic, Cole, Luiz, Cahill, Terry, Azpilicueta, Bertrand, Ramires, Lampard, Oscar, Mikel, De Bruyne, van Ginkel, Hazard, Willian, Torres, Mata, Schurrle, Ba, Eto'o
Manchester City: Hart, Pantilimon, Johansen, Richards, Kompany, Zabaleta, Lescott, Kolarov, Clichy, Demichelis, Nastasic, Boyata, Milner, Nasri, Garcia, Navas, Rodwell, Silva, Fernandinho, Toure, Negredo, Dzeko, Aguero, Jovetic
Manchester United: De Gea, Lindegaard, Rafael, Evra, Jones, Ferdinand, Evans, Smalling, Vidic, Fabio, Buttner, Anderson, Giggs, Carrick, Nani, Young, Cleverley, Valencia, Kagawa, Zaha, Fellaini, Rooney, Hernandez, Welbeck, van Persie
Celtic: Forster, Zaluska, Izaguirre, Ambrose, van Dijk, Wilson, Mulgrew, Mouyokolo, Lustig, Biton, Brown, Commons, Ledley, Rogic, Samaras, Stokes, Boerrigter, Balde, Pukki
*Zingatia; vikosi vyote vimeambatanishwa na vikosi vya timu B, vinavyohusisha wachezaji wa umri usiozidi miaka 21

0 comments:

Chapisha Maoni