The reliable source of sport news

Alhamisi, Septemba 05, 2013

VAN PERSIE AMESISITIZA ANAFURAHA KUFANYA KAZI NA MOYES, AMEKANUSHA HABARI KWAMBA HAFURAHII UONGOZI WAKE SI ZA KWELI

5.9.13 By Unknown No comments

Van Persie akielekwzwa jambo na David Moyes
Robin van Persie amekanusha madai kwamba hana furaha kufanya kazi chini ya meneja mpya wa Manchester United, David Moyes.

Mshindi huyo wa kiatu cha dhahabu misimu miwili mfululizo iliyopita, Robin van Persie alipata ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa chini ya Sir Alex Ferguson aliyekuwa akitumikia msimu wake wa mwisho Old Trafford.
Mdachi huyo ameanza vema pia msimu huu, alifanikiwa kuzamisha mipira miwili wavuni Manchester United iliposhinda Ngao ya Jamii dhidi ya Wigan na magoli mengine mawili kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Swansea.
Van Persie tangia hapo hajafunga tena. Hakufanikiwa kupata nafasi ya kufanya chochote pale walipotoa sare dhidi ya Chelsea na mechi ya Jumapili iliyopita dhidi ya Liverpool walipotoka Anfield mikono ikiwa chini kwa kichapo cha bao 1-0.
Na uvumi umetapakaa ukidai kuwa Van Persie hafurahii mfumo wa ufundishaji David Moyes.
Lakini mdachi huyo mwenye umri wa miaka 30 amesisitiza kuwa habari hizo si za kweli kabisa, amekaririwa akisema: “Ni jambo kubwa kwangu kufanya kazi na meneja mpya David Moyes. Ana aina na mbinu mbalimbali za ufundishaji, nazipenda.
“Namfurahia Moyes. Anafundisha, yuko karibu na wachezaji na wafanyakazi wengine pia, anatuandaa vema kwa mechi inayofuata. Na hilo linatuleta pamoja.
“Kwa bahati njema, ushindi wa ubingwa msimu uliopita umetupa njaa ya kutaka tena.”
Robin van Persie alikuwa lulu kwa Manchester United mwaka jana kipindi cha usajili, lakini David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson ameshindwa kuleta mchezaji nyota Old Trafford.
Hatimaye United imefanikiwa kumyakua mchezaji wa kimataifa raia wa Ubelgiji Marouane Fellaini kutoka Everton dakika za majeruhi kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Lakini vilevile waliwakosa wachezaji wengine waliokuwa kwenye rada yao wakiwamo, Cesc Fabregas, Leighton Baines, Ander Herrera, Cesc Fabregas, Sami Khedira na Fabio Coentrao.

Manchester United walikuwa na shauku ya kumleta Marouane Fellaini kabla ya dirisha la usajili kufungwa, na walifanikiwa kumnasa kwa kitita cha paundi milioni 27.5.

0 comments:

Chapisha Maoni