Cesc Fabregas amewaambia marafiki zake kwamba anataka kurudi tena kwenye klabu yake ya zamani endapo atarudi tena kwenye Ligi ya Uingereza. Nahodha huyo wa zamani wa The Gunners aliondoka Emirates msimu wa majira ya joto wa 2011. Fabregas bado anaendelea kuwasiliana kwa ukaribu sana na bosi Arsene Wenger na imeripotiwa wawili hao wamekuwa wakiwasiliana mara kwa mara. Chanzo: Mirror Football
Liverpool inaweza kupata upinzani katika harakati zao kumsajili Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Bernard toka kwa Tottenham Hotspur ambao nao pia wanavutiwa na winga huyo.Ripoti zinasema kwamba Brendan Rodgers na Adre Villas Boas wanataka kumsajili kiungo huyo wa Atletico Mineiro lakini vile vile wanapata upinzani toka Porto, Shakhtar Donetsk na Borussia Dortmund ambao wote wako tayari kutoa dau kwa mchezaji huyo. Chanzo: The Independent
Wakati Luis Suarez akiwa tayari kuvunja ahadi yake aliyoweka wakati aliposema kwamba hatajiunga na klabu nyingine yoyote ya ligi ya Uingereza, amejikuta akitaka kusaini mkataba Arsenal. Matumaini ya Arsenal kumpata nyota huyo yanaongezeka na kuna uwezekano wakaongeza dau lao ili kujihakikishia kwamba wanapata huduma yake baada ya ofa ya kwanza kutupiliwa mbali na Liverpool. Source: Mirror Football
Manchester United imejikuta ikivunjika moyo katika jitihada zake kumsajili Cesc Fabregas kufuatia Barcelona kuona ni upuuzi mtupu maombi hayo ya Manchester United na kudai kwamba nyota huyo haondoki Camp Nou, makamu wa rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ametilia mkazo na kusema: “Barca will not entertain any offers for Cesc. He is non-transferable.” Source:Mail Online
Goli kipa wa QPR goalkeeper Julio Cesar ameshauriwa kupunguza malipo anayodai kulipwa endapo atajiunga na Arsenal ili kuweza kujiunga na klabu hiyo. Arsene Wenger amekatishwa tamaa na fedha anayotaka kulipwa mchezaji huyo ambaye anataka alete upinzani Emirates kwa Wojciech Szczesny na Lukasz Fabianski. Source: The Metro




0 comments:
Chapisha Maoni