Luis Suarez anapaswa kuiambia klabu yake ya Liverpool kwamba anataka uhamisho wa majira ya joto kwenda Arsenal kwa mujibu wa habari toka Jarida la The Mirror.
Mustakabali wa raia huyo wa Uruguay umekuwa gumzo Anfield kipindi hiki, na hasa wakati mshambuliaji huyo alipoweka wazi hapo awali kwamba anatamani kwenda Real Madrid.
Lakini wababe hao wa La Liga walishindwa kukidhi azma yake hiyo, jambo ambalo liliacha mlango wazi kwa Arsenal. Washika mtutu Arsenal wako sokoni kusaka mchezaji atakayeboresha safu ya ushambuliaji, na inasemekana wamebadili dhamira yao ya kumsajili nyota wa Real Madrid Gonzalo Higuain na kumgeukia Suarez na hivyo kufikia hatua ya kupanda dau la pauni milioni 30 wiki iliyopita.
Liverpool wanatambua kwamba itakuwa vigumu kumshawishi nyota huyo kubaki klabuni ingawa wanakabiliwa na maombi hayo ya uhamisho wakati wameshamjumuisha kwenye kikosi kinachofanya maandalizi ya kuanza msimu. Ingawa Liverpool hawahitaji kumuachilia nyota huyo, Arsenal wanaamini kwamba dau la pauni milioni 40 linaweza kuwarusha roho wapinzani wao wa Anfield.




0 comments:
Chapisha Maoni