Metro wameeleza kuwa Arsenal wanaweza kufanya uhamisho wa Mbrazili Luiz Gustavo baada ya Bayern Munich kuweka wazi kwamba mchezaji huyo anaweza kuondoka msimu huu wa kiangazi.
Wakati tetesi nyingi ziliihusisha Arsenal na usajili wa washambuliaji bora watakaoleta mabadiliko klabuni hapo, Wenger anaonekana kutaka kumsajili nyota huyo raia wa Brazili ili kuboresha safu yake ya ulinzi, hasa sehemu ya kati.
Bayern Munich watamuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye ameichezea timu yake ya taifa mara 10 wakati huo Javier Martinez akitarajiwa kuchukua nafasi yake. Pia klabu hiyo haina wasi wasi wowote endapo ataondoka kufuatia usajili wa Thiago Alcantara ambaye ataleta ladha klabuni hapo tunapoelekea kuanza msimu mwingine.
Kwa upande wa Bundesliga Wolfusburg nayo inajipanga kutoa dau kwa mchezaji huyo wa zamani wa Hoffenheim wakati akioneshwa mlango wa kutoka Allianz Arena baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha mwishoni mwa msimu uliopita.
Ingawa Gustavo mwenyewe ameeleza kwamba hajasikia chochote toka kwa timu nyingine lakini amekiri kwamba anaweza kushawishika kuondoka kwa mwajiri wake majira ya joto. Alisema " Sijui chochote kuhusu tetesi" aliiambia Goal.com "Hakuna yeyote aliyeongea na mimi. Tunasubiri tuone nini kitatokea."
Mkataba wa Gustavo na miamba hao wa Bavaria utafikia tamati mwaka 2015 lakini Bayern inaweza kukubali kupunguza ada ya usajili hadi pauni milioni 8 jambo ambalo linaweza kuwavutia Washika mtutu.




0 comments:
Chapisha Maoni