Mchezaji wa Kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amehusishwa mara kadhaa na tetesi za kuihama klabu yake lakini amesema wazi ana furaha kubaki Santiago Bernabeu
Cristiano Ronaldo ana furaha kuwa Real Madrid na hana mpango wa kuondoka kwenda Manchester United kama ulivyokuwa uvumi wa habari.
Mreno huyo alisema mapema wiki hii kwamba analimis soka la Ligi ya Uingereza, lakini ameweka mambo bayana kwamba hana mpango wa kurejea tena kwenye ligi ya Uingereza ama Manchester United msimu ujao.
Mreno huyo alisema mapema wiki hii kwamba analimis soka la Ligi ya Uingereza, lakini ameweka mambo bayana kwamba hana mpango wa kurejea tena kwenye ligi ya Uingereza ama Manchester United msimu ujao.
"Manchester United ni klabu iliyokuwa moyoni mwangu tangu kipindi nilipokuwa nacheza pale, kila mmoja natambua kwamba nina mapenzi na klabu hii. Lakini mustakabali wangu uko Madrid na ninataka kubaki hapa, Ronaldo alimwambia mwanahabari wa Goal.com.
"Leo si siku ya kuongelea mustakabali wangu.Nitazungumzia hayo kabla ya msimu kuanza. Kimsingi huu ni muda wangu kupumzika baada ya kucheza msimu mrefu wa miezi 10.
"Nafurahi kucheza hapa, Nimekuwa nikicheza ligi ya Hispania miaka minne sasa na bado nahitaji kuendelea.
"Kuhusu timu yangu ya taifa natumaini tutafuzu kucheza kombe la dunia - itakuwa mafanikio makubwa kwetu, naisubiri michuano ya kombe la dunia kwa shauku kubwa.
"Ki ukweli napenda kufanya vizuri daima, msimu huu naamini nitafanya vema pia. Nitajitahidi kuhakikisha tunashinda ubingwa wa La Liga na klabu bingwa Ulaya pia."
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 201 katika mechi 199 alizocheza Madrid tangu alipojiunga na Klabu hiyo Majira ya Joto mwaka 2009. Ronaldo ana mkataba na los Blancos hadi 2015.




Jembe hilo
JibuFuta