ASILIMIA 100 GUNNERS: Rekodi ya Arsenal mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa
Imecheza mechi 11, imeshinda 11, imefunga mabao 27, imefungwa 3
2006-07 - Dinamo Zagreb (ugenini) 3-0, Dinamo Zagreb (nyumbani) 2-1
2007-08 - Sparta Prague (ugenini) 2-0, Sparta Prague (nyumbani) 3-0
2008-09 - Twente (ugenini) 2-0, Twente (nyumbani) 4-0
2009-10 - Celtic (ugenini) 2-0, Celtic (nyumbani) 3-1
2011-12 - Udinese (nyumbani) 1-0, Udinese 2-1 (ugenini)
KLABU ya Arsenal imepunguza 'pasua
kichwa' kwa mashabiki wake baada ya kuondoka Uturuki na ushindi mnono wa
mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza Ligi ya
Mabinghwa Ulaya.
Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo
Kieran Gibbs dakika ya 51, Aaron Ramsey dakika ya 64 na Olivier Giroud
aliyefunga kwa penalti dakika ya 77 na kumpa tabasamu pana kocha
anayepigiwea kelele kwa ubakhili wa kutosajili, Mfaransa Arsene Wenger.
Laurent Koscielny alilazimika kutoka nje
kipindi cha kwanza baada ya kupasuka karibu na jicho lake baada ya
kupigwa buti na Pierre Webo.
Kikois cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny/Jenkinson dk33, Gibbs, Rosicky, Wilshere, Ramsey, Cazorla, Giroud na Walcott/Monreal. dk87.
Fenerbahce: Demirel, Irtegun/Gonul dk46, Yobo, Bruno Alves, Kadlec, Topal, Meireles/Potuk dk82, Emre, Sow, Webo/Emenike dk62 na Kuyt.
Imepunguza presha: (kutoka kushoto) Carl
Jenkinson, Kieran Gibbs, Theo Walcott, Aaron Ramsey na Olivier Giroud
wakishangilia bao la kwanza

Ramsey akiifungia Arsenal bao la pili

Olivier Giroud akiifungia Arsenal bao la tatu kwa penalti baada ya Theo Walcott kuchezewa rafu na Michal Kadlec kwenye boksi

Per Mertesacker, (wa pili kushoto)
Jenkinson (wa tatu kushoto) na Walcott (wa tatu kulia) wakimkimbilia
mfungaji Giroud (katikati)

Arsene Wenger akilalamika baada ya
Laurent Koscielny (anayegaagaa chini) kupigwa teke usoni na Pierre Webo.
Mshambuliaji huyo wa Fenerbahce alipewa kadi ya njano

Koscielny akipigwa buti usoni na Webo

Koscielny alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Carl Jenkinson na Arsenal ilipata pigo lingine

Jack Wilshere akiwa chini kipindi cha kwanza baada ya kuumizwa

Wilshere alirejea uwanjani na kuendelea kutawala sehemu ya kiungo ya Arsenal




0 comments:
Chapisha Maoni