SI kitu ambacho unaweza kuwaona makocha wa Ligi Kuu ya England wakifanya. Vema, si mbele ya kamera, popote.
Picha za kuzindua msimu za Bayern
Munich, zinawaonyesha mabingwa hao wa Ulaya wakionja pombe aina ya
Oktoberfest baada ya kuanza msimu kwa kishindo.

Mambo hayo: Kocha Pep Guardiola (mbele kushoto) na Mspanyola, Javi Martinez (chini kulia) wakifurahia Paulaner

Mtungi: Mabingwa wa Ujerumani na Ulaya wakifurahia mwanzo mzuri Bundesliga
Kocha mpya, Pep Guardiola aliyehamia
Ujerumani kutoka Hispania, anaonekana aliye vizuri tu akifurahia
Paulaner lager, akiwa na kikosi chake katika vazi la asili la Ujerumani.
Ni mavazi ambayo kwa watu kama Bastian
Schweinsteiger na Phillip Lahm wameonekana mara kadhaa wakiwa wamevaa
kabla, lakini kwa watu wapya Guardiola, Thiago Alcantara na Mario Gotze,
hii ilikuwa mara ya kwanza na walipendeza.
Guardiola ameanza msimu kwa kipigo cha
mabao 4-2 katika Super Cup ya Ujerumani kutoka kwa Dortmund, lakini
akashinda mechi mbili mfululizo za Bundesliga, 3-1 dhidi ya Borussia
Monchengladback na 1-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt Jumamosi.


Mtu mpya: Guardiola (kushoto) akifurahia
kaka ilivyo kwa mchezaji mpya Mario Gotze (kulia) baada ya kutua
akitokea Borussia Dortmund majira ya joto

Mabingwa: Bayern imeanza kutetea ubingwa wa Ujerumani, Bundesliga kwa kushinda mechi mbili mfululizo

Inua glasi: Guardiola na benchi lake zima la ufundi watatumai kuendeleza wimbi la mafanikio msimu huu
Timu ya Bayern walifurajia na majagi na
bia hizo mbili za Ujerumani, na kusherehekea kushinda taji
Bundesliga-msimu uliopita kwa kumwagiana lita za bia Allianz Arena kabla
ya kupokea taji la 23 la ubingwa wa Ujerumani.
Lakini kiungo Franck Ribery, ambaye ni
muislamu safi, hakuwa mwenye furaha sana. Bahati nzuri kwake ni kwamba
bia hiyo haikuwa na kilevi, na Mfaransa huyo alipigwa picha akiwa
ameshika bia hiyo.

Mataji: Wachezaji wa Munich wakishereheeka na taji la Bundesliga baada ya kutwaa msimu uliopita

Chukua hiyo: Bastian Schweinsteiger akimwagiana na bia na mchezaji mwenzake, Daniel van Buyten

Franck Ribery akiogeshwa bia





0 comments:
Chapisha Maoni