BAADA ya kutua kwa mkopo Liverpool, Aly Cissokho amesema kwamba sasa ni wakati wa kupiga mzigo wa uhakika Anfield.
Beki
huyo wa kushoto wa Valencia ametambulishwa na Wekundu hao na
anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Aston Villa Jumamosi.
Anakwenda
kuchukua nafasi ya Jose Enrique katika safu ya ulinzi ya Anfield katika
harakati za kocha Brendan Rodgers kusuka kikosi kamambe kitakachompa
tiketi ya Ligi ya Mabingwa.
VIDEO Kaangalie video chini

Tayari kwa kazi: Aly Cissokho amesema yuko kuanza kazi Liverpool baada ya kutua akitokea Valencia kwa mkopo
Cissokho,
ambaye atavaa jezi namba 20 alisema: "Najisikia furaha kwa kiasi
kikubwa kuwa hapa na najivunia kazi ngumu niliyofanya hadi kufika hapa
katika soka yangu.
"Wakati
wote nimekuwa nikiota kusaini klabu gwiji. Nimekuwa mwenye bahati kiasi
cha kutosha kuchezea klabu chache na kwa sasa kupata nafasi ya kuchezea
klabu kama Liverpool, ni babu kubwa.
"Wakati
wote nimesema, mbali na kuwapo wachezaji wengi wa Ufaransa, kwamba
napenda haswa Ligi ya England, na pia nimekuwa na bahati kiasi cha
kutosha kuchezea klabu fulani kubwa, katika fikra zangu nyuma, wakati
wote nilitaka kucheza England.

Anasaini: Beki wa kushoto, Cissokho atavaa jezi namba 20 Anfield
Cissokho
tayari amecheza Anfield, baada ya kuwamo katika kikosi cha Lyon
kilichoshinda 2-1 katika hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya
mwaka 2009.

Mazoezini: Cissokho (kulia kabisa) ameungana na wachezaji wenzake wapya Liverpool kukimbia Melwood

Ally Cissokho anatarajiwa kugombea namba na Jose Enrique katika beki ya kushoto


Wa mkopo: Cissokho amewasili Anfield kupiga kazi kwa muda akitokea Valencia

Makocha wa Liverpool wakimuangalia mchezaji mpya, Cissokho katika Uwanja wa mazoezi Melwood

Tabiri, nani yuko nyuma? Wachezaji wa Liverpool akiwemo Luis Suarez wakiwa na mchezaji mpya, Cissokho wakati wa mazoezi mepesi



0 comments:
Chapisha Maoni