CRISTIANO
Ronaldo ameikaba koo Real Madrid. Anafahamu wazi, rekodi yake ya
uhamisho wa Pauni 80 milioni inayoshikilia dunia kwa sasa itavunjwa na
Gareth Bale na hivyo sasa ametafuta namna ya kuendelea kuwa na hadhi
kubwa katika klabu hiyo.
Supastaa
huyo wa Ureno, amesema atakubali kuendelea kubaki Santiago Bernabeu na
kucheza sambamba na Bale kama tu atalipwa mshahara wa Pauni 320,000 kwa
wiki.
Ronaldo
bado anataka kubaki nchini Hispania, licha ya kuhusishwa na mpango wa
kujiunga na Manchester United na Paris Saint-Germain.
Akitambua
rekodi yake itavunja, Ronaldo sasa ametaka kulipwa mara mbili ya
mshahara atakaolipwa Bale ili aendelee kuwa namba moja kwa wachezaji
wenye hadhi kubwa katika klabu hiyo ya Hispania.
Sambamba
na hilo, Ronaldo anatarajia klabu yake kumpigia kampeni za nguvu katika
mchakato wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia na anataka pia
kupatia fursa za kibiashara atakazofungua Asia na Amerika.
Baada ya
kufunga mabao 175 katika mechi 167 alizochezea Real Madrid, Ronaldo
anataka mshahara wake upande kwa kasi, licha ya mkataba wake kubakiza
miaka miwili.
Suala
hilo sasa linatarajiwa kuwafanya mabosi wake waanze kukuna kichwa
kuhusiana na namna ya kutekeleza matakwa yake ili kumkutanisha na Bale
kikosini:CHANZO MWANASPOTI




0 comments:
Chapisha Maoni