KOCHA Arsene Wenger yuko katika siku 12
ngumu za kukimbizana kukamilisha usajili kabla ya dirisha kufungwa na
sasa amehamishia ndoana zake kwa Mathieu Flamini, kiasi cha miaka mitano
tangu aondoke Arsenal kuhamia AC Milan.
Klabu hiyo ya Italia imemtema mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 29 mwishoni mwa msimu na sasa kiungo huyo
kiasi cha wiki mbili amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha Wenger.
Kocha wa Arsenal amevutiwa kiasi cha
kutosha na hali ya mchezaji huyo na yuko tayari kumpa ya Mkataba Flamini
baada ya kukubali kurejea nyumbani licha ya kutakiwa na klabu nyingine.

Wameungana tena: Akiwa amiechezea zaidi ya mechi 100 The Gunners, Flamini aliondoka Arsenal kuhamia AC Milan mwaka 2008
Atakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na
Wenger majira haya ya joto— wote wachezaji huru — na mchezaji wa nne wa
zamani wa timu hiyo kusainiwa tena na kocha huyo, baada ya awali
kuwarejesha Sol Campbell, Jens Lehmann na Thierry Henry Emirates.
Wenger anatumai dili hilo litafuatiwa na usajili wa mchezaji mqwenye jina kubwa katika klabu hiyo.
Mshambuliaji wa Real Madrid, Karim
Benzema ni mchezaji anayetakiwa zaidi kwa sasa na Wenger baada ya
kushindwa kuwapata Luis Suarez au Wayne Rooney.
Na Mfaransa huyo pia ametenga dau kubwa
zaidi kwa ajili ya mchezaji mwenzake Benzema, Angel Di Maria, na pia
atarajea na ofa nzuri zaidi kwa ajili ya kiungo wa Newcastle Yohan
Cabaye na kipa wa Valencia, Vicente Guaita.
Mchezajhi mmoja tu ambaye anaweza kuondoka kwa sasa ni Lukas Podolski, ambaye anatakiwa na Schalke.

Kijana wa zamani wa Arsenal: Thierry
Henry alitangaza kurejea klabu hiyo na kufunga bao katika Kombe la FA
dhidi ya Leeds mwaka 2012


Jens Lehmann na Sol Campbell pia walijiunga tena na timu ya Arsene Wenger baada ya kuhama
Real itataka dau la jumla la Pauni
Milioni 60 ili kuwauza wote Benzema na Di Maria. Newcastle inataka
angalau Pauni Milioni 20 kwa Cabaye, wakati Guaita imeelezwa ni kiasi
cha Pauni Milioni 25.6 kuvunja Mkataba wake.



0 comments:
Chapisha Maoni