MWANASOKA
bora wa dunia, Lionel Messi jana alifunga mabao mawili na kutengeneza
lingine kuwasaidia Neymar na kocha wa Barcelona, Gerardo Martino kuanza
kazi vizuri kwa ushindi wa 7-0 dhidi ya Levante kwenye Ligi Kuu ya
Hispania.
Katika
mchezo huo ambao Neymar alianzia benchi, mabao ya Barca yalifungwa na
Sanchez dakika ya tatu, Messi dakika ya 12 na 42 kwa penalti, Alves
dakika ya 23, Pedro dakika ya 26 na 73 na Xavi dakika ya 45.
Kikosi
cha Barcelona kilikuwa: Valdés, Alves, Piqué, Mascherano, Adriano,
Fàbregas, Busquests, Xavi, Pedro/Tello, Alexis/Neymar, Messi/Iniesta.
Levante:
Navas, Navarro, Rodas, Barral, El Zhar, Rubén, Juanfran, Xumetra,
Sergio, Pedro López na Simao.

Watching
on: £50m wonderkid Neymar started the match from the bench

Big
entrance: Neymar was a second half substitute but Barca had already
taken their foot well off the gas by then

In
action: Neymar wasn't able to get on the score sheet
Nayo
Real Madrid imeanza vyema mbio zake za La Liga kwa ushindi mwembamba wa
2-1 dhidi ya Real Betis.
Jorge
Molina aliwatuliza mashabiki Uwanja wa Bernabeu kwa bao la dakika ya
15, kabla ya Karim Benzema kusawazisha dakika 10 baadaye na mchezaji
mpya, Isco akafunga la ushindi dakika ya 86.
Kikosi
cha Real Madrid kilikuwa: Lopez, Pepe, Ramos, Khedira/Casemiro,
Ronaldo, Benzema/Morata, Özil/Di Maria, Marcelo, Carvajal, Modric na
Isco.
Real
Betis: Andersen, Chica, Perquis, Paulao, Nacho, Matilla, Nosa, Verdú,
Juanfran, Cedrick na Molina.

Shujaa:
Isco ameifungia bao la ushindi dakika za lala salama Real Madrid

Ametoka
kapa: Cristiano Ronaldo alipata nafasi kadhaa za kufunga, lakini
akapoteza



0 comments:
Chapisha Maoni