MSHAMBULIAJI
Wayne Rooney hatimaye amekubaliana na ukweli kwamba hawezi kuruhusiwa
kuondoka Manchester United kujiunga na Chelsea.
Licha
ya kuonyesha nia ya kutaka kwenda kuchezea timu ya Jose Mourinho,
Rooney ameamua kutulia ili awe fiti kabisa, baada ya kukosa mechi za
kujiandaa na msimu na United kutokana na kuwa majeruhi.
Mshambuliaji
huyo alicheza kwa mara ya kwanza chini ya kocha mpya, David Moyes
katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu jana timu yake ikishinda 4-1 dhidi
ya Swansea lakini, akatengeneza mabaso mawili baada ya kuingia akitokea
benchi kipindi cha pili.
Rooney hakwenda hata kushangilia na wachezaji wenzake mabao hayo.
Hana
habari: Rooney (wa nane kulia) akizungumza na refa Phil Dowd wakati
wachezaji wenzake wa United wakishangilia na Danny Welbeck baada ya
kufunga bao lililohitimisha ushindi wa 4-1
Alishuhudia
akiwa benchi wakati Robin van Persie akifunga bao la kwanza na Danny
Welbeck akifunga la pili, lakini akaingia uwanjani dakika ya 62.
Rooney
alikwenda kutengeneza bao la kwanza kipindi cha pili lililofungwa na
Van Persie kabla ya kumtengenezea pia Welbeck nafasi ya kufunga bao la
nne, lakini alijitenga kabisa wakati wenzake wanashangilia mabao hayo.

Amesalimu amri: Rooney ataendelea kuwa mchezaji wa Manchester United msimu huu

Chini
ya maelekezo: Rooney aliingia uwanjani dakika ya 61 kuchukua nafasi ya
kocha mchezaji, Ryan Giggs na kutengeneza mabao mawili
"Wayne amekuwa akifanya mazoezi kwa bidii, kwa sababu anataka kurudi kikosini,"chanzo kimesema.
"Nafikiri
amekiri hakuna namna klabu inaweza ingeweza kumuuza na ameamua
kuendelea kufanya mazuri kama aliyofanya. Haitachukua muda mrefu kurudi
kikosi cha kwanza,".

Anaangalia mchezo: Rooney akiwa ameketi na Wilfrid Zaha na Chris Smalling katika benchi la United jana
Baada
ya mchezo wake huo wa kwanza wa Ligi Kuu England, David Moyes alisema:
"Tumeweka mambo sawa. Wayne anajituma sana [mazoezini] na kwa mchezaji
yoyote, unapovuka mstari wa kuingia uwanjani, unakwenda kucheza soka
yako.’





0 comments:
Chapisha Maoni