KLABU ya Liverpool imekaa katika mkao wa
kula saini ya Willian na kuzipiku Tottenham na Manchester United ambazo
pia zinawania saini ya mchezaji huyo mwenye thamani ya Pauni Milioni
30.
Zote Liverpool na Tottenham zimeingia
kwenye mazungumzo na Anzhi Makhachkala kwa ajili ya mwanasoka huyo wa
kimataifa wa Brazil, lakini inatokea Willian amekaa kwenye mkao wa
kuelekea zaidi Anfield.
Ikiwa Liverpool itakamilisha uhamisho wa
mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, Willian atakuwa mchezaji wa pili
katika klabu hiyo kihistoria na atakuwa mchezaji babu mkubwa ambaye
amesajiliwa na kocha Brendan Rodgers majira haya ya joto.
Na itakuwa na maana kubwa kwa Liverpool,
kuwapiga bao wapinzani wao wakubwa Manchester United pamoja na
Tottenham, ambao wanamtamanisha kucheza michuano ya Ulaya ili avutike
zaidi kusaini kwao.
Willian ameaiambia ESPN Brazil, baada ya
kuambiwa Liverpool inamtaka mapema wiki hii kwamba; 'ametulia sana na
anasubiri kilicho bora' na pia akaitaka Liverpool kama klabu kubwa.

Anamtaka: Brendan Rodgers anaweza kutoa Pauni Milioni 30 kumuingiza mchezaji huyo kikosini Liverpool
Rodgers amekuwa akipambana kuboresha
kikosi chake kutafuta viwango vya kuiwezesha timu kufuzu michuano ya na
kuwasili kwa Willian, ambaye alishinda Kombe la UEFA enzi zake
akiichezea Shakhtar Donetsk, kunaweza kusababisha hali hiyo.
Liverpool pia itamsajili beki wa kushoto anayecheza kwa mkopo wa muda mrefu Valencia, Aly Cissokho akifuzu vipimo vya afya.

Wanamkosa: David Moyes amekula za uso sana katika dirisha la usajili majira haya ya joto




0 comments:
Chapisha Maoni