MSHAMBULIAJI Wayne Rooney amerejea
mazoezini kikosi cha kwanza Manchester United kabla ya mechi ya kwanza
ya mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Swansea.
Rooney aliichezea England ikishinda wa
3-2 dhidi ya Scotland Jumatano, alionekana yuko fiti na tayari kufanya
kazi kwenye kikosi cha David Moyes katika mechi ya kwanza ya ushindani.
Mshambuliaji huyo bado anahusishwa na
mpango wa kuondoka Old Trafford, huku wapinzani wa United katika Ligi
Kuu, Chelsea wakiwa mstari wa mbele kutaka kumsajili.
VIDEO Nenda chini kuangalia Gerrard akimzungumzia Rooney

Nyuma ya kioo: Mustakabali wa Rooney bado haueleweki, akihusishwa kutimkia Chelsea
Amehusishwa kwenye kikosi cha David
Moyes kuelekea mchezo huo, lakini Rafael na Javier Hernandez wote
majeruhi wa nyama za paja na mawinga waili, Nani na Ashley Young
wanatarajiwa kuwa nje.
Wilfried Zaha anajiandaa kucheza mechi
yake ya kwanza ya Ligi Kuu, wakati Michael Carrick anatarajiwa kupona
maumivu ya jichos aliyoyapata akiichezea England mechi ya kirafiki.
Rooney amekuwa nje ya kikosi cha United
wakati wa kujiandaa na msimu kutokana na maumivu ya bega, na baada ya
kumuona akiichezea nchi yake, Moyes amemjumuisha mchezaji huyo kwenye
kikosi cha mabingwa hao wa Ligi Kuu, huku akisistiza hauzwi.
"Hakuna maendeleo zaidi na hatutaki chochote, kwa sababu tumekwsihamuambia kila mtu hauzwi," alisema Moyes.
"Nitahitaji kuona, yukoje atakaporejea.
Nitajaribu na kumfautilia. Nimeona mchezo usiku wa juzi, nafikiri kwa
dakika 65 alizocheza alifanya vizuri, anazunguka na anaonekana yuko
fiti.'

Hatimaye kazini...: Wayne Rooney alicheza mechi yake ya kwanza wakati wa kujiandaa na msimu, England ikishinda dhidi ya Scotland

Kwenye kipaza: Kocha wa United, David Moyes anasistiza Rooney hauzwi





0 comments:
Chapisha Maoni