The reliable source of sport news

Ijumaa, Agosti 23, 2013

Lukas Podolski kutimkia zake Schalke kwa mkopo

23.8.13 By Unknown No comments

Mchezaji wa Arsenal  Lukas Podolski yuko kwenye mazungumzo na Schalke kwa ajili ya uhamisho wa mkopo kwa mujibu wa London Metro.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Ujerumani aliwasili Emirates kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 10 msimu uliopita akitokea Cologne, lakini baada ya kusota akitafuta namba kikosi cha kwanza sasa mlango umemfungukia kwa uhamisho wa muda wa mkopo.
Bosi wa The Gunners, Arsene Wenger atamruhusu Podolsk kuondoka Emirates kwasababu anataka kujitengenezea nafasi kwa ajili ya kombe la dunia litakalochezwa mwaka 2014 huko Brazil, kwasababu hawezi kumhakikishia nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza mara zote kwenye Ligi ya Uingereza.
Schalke iko tayari kuilipa Arsenal paundi 100,000 ikiwa ni ujira wa wiki kwa 2013/14, kwahiyo nyota huyo atakuwa amebakiwa na miaka miwili kwenye mkataba wake na Arsenal.
Pamoja na timu nyingine kama  Galatasaray na Tottenham Hotspur kumhitaji lakini nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich atachagua kurudi nyumbani ambako amekuwa akicheza kwa kipindi chake chote kwenye soka.
Wakati Spurs na Galatasaray zikiwa zinahitaji kumsajili Podolski kwa mkataba wa kudumu, uhamisho wa mkopo kwenda Schalke unaonekana ni bora zaidi kwa Klabu na mchezaji pia kwasababu itakuwa ni rahisi kurudi Arsenal tena msimu ujao.

0 comments:

Chapisha Maoni