The reliable source of sport news

Jumanne, Agosti 13, 2013

Barua ya mapenzi ya Ferguson: Aeleza Upenzi wake kwa Premier Ligue

13.8.13 By Unknown No comments

Mpira wa miguu haukubaki kama ulivyokuwa mwanzo tangu Sir Alex Ferguson alipotangaza kustaafu kuwa meneja wa Manchester United mwishoni mwa msimu uliopita.
Kilikuwa ni kipindi kingine cha kufurahisha kwa mashabiki wa mpira wa miguu siku ya Jumapili wakati waliposhuhudia Mashetani hao wekundu wakinyanyua taji linguine bila ya kocha wao maarufu Ferguson. Hata hivyo, wale wote wanaomis uwepo wake msimu huu wa majira ya joto, watakuwa na shauku kubwa kusikia kile ambacho mzee huyu maarafu katika historia ya mpira wa miguu ameandika kuhusu upendo wake kwa Barclays Premier League.
Enzi zake Manchester United - Kitendo cha kutangaza kustaafu ukocha kiliwashtua mashabiki wengi

Akiongea kuhusu uzoefu wake kwenye gemu, wakati akiongoza moja ya klabu kubwa za mpira wa miguu duniani kwa takribani miaka 27, Mscotish huyo anazungumzia hali ya michezo katika ulimwengu wa kisasa.
Haya ndiyo maneno aliyoandika kuhusu Ligi ya Uingereza, endelea kusoma upate maneno yake kamili.

Mpira wa miguu umekuwa maisha yangu na nimepata fursa ya kuwa na klabu bora sana Manchester United.
Mashabiki, wachezaji, wafanyakazi wenzangu – wote wameshiriki kufanya kitu Fulani cha kukumbukwa. Mataji tuliyoshinda, magoli bora toka kwa wachezaji, mechi za kuvutia tulizocheza, na michezo yote tuliyopoteza vyote navikumbuka sasa – yote yanapaswa kuwa kwenye kumbukumbu klabu iliyofanya kwenye Mpira wa miguu wa Uingereza.
Ferguson anakiri kwamba, Mpira wa miguu umekuwa sehemu ya maisha yake na amefurahia mafanikio yake



Mambo mengi yamebadilika katika michezo tangu nilipowasili toka Aberdeen Novemba 1986, ikiwa ni pamoja na upenzi na kiwango cha uelewa. Kumekuwa na mabadiliko kutoka msimu mmoja hadi mwingine. Lakini kuna mabadiliko kwa ujumla kwenye Ligi ya Uingereza ukilinganisha na miaka 27 iliyopita.
Katika ligi mbalimbali, viwanja vya michezo si kama ilivyokuwa zamani, maendeleo ya wachezaji hayakuwa kama ilivyo sasa, waliokuwa wakirusha habari za michezo hawakuweza kurusha moja kwa moja kwenye TV kama ilivyo sasa, mashabiki hawakuwa wakisikilizwa na serikali zilikuwa zikipishana na michezo.
Alipoteuliwa: Sir Alex Ferguson amekiri kwamba Mchezo wa mpira una sura mpya kuliko alipowasili Old Trafford



Manchester United, labda zaidi ya klabu nyingine yoyote, imeleta chachu ya mabadiliko katika michezo Uingereza katika muda wote wa Ligi ya Uingereza. Uwajibikaji wa klabu katika kuwekeza katika kila Nyanja kunaiwezesha kung’ara. 
Wachezaji wa kiwango cha juu wote wamechangia kununua na kuendeleza mali za Old Trafford na Carrington kwa wachezaji na mashabiki; Mipango ya kijamii inatuunganisha na jamii kwa maendeleo ya sasa na baadaye – klabu imejiweka katika hali ambayo kila klabu katika ligi ya Uingereza inapambana kuifikia, mara nyingine zinafanikiwa kufika.



Changamoto zinazojitokeza msimu baada ya msimu, zinatufanya tujitahidi kufanya vizuri zaidi ya mwanzo. Katika kipindi changu wapinzani walipanda na kushuka. Wengine wamebaki na wengine wanaendelea kupambana. Lakini upinzani ndiyo afya na ndicho kinachoipa ligi hii ladha kuliko ligi nyingine za Ulaya.
Tunatambua kwamba hakuna timu inayotaka kushindwa, Ubora wa Ligi ya Uingereza umekuwa ukiongezeka mwaka kwa mwaka. Haikuwa kitu rahisi kutwaa ubingwa, kupata mchanganyiko mzuri wa wachezaji – vijana wanatofautiana fikara.
Mfano Halisi: Ferguson ameshiriki kukuza vipaji, kama Cristano Ronaldo ambaye ni miongoni mwa wachezaji bora sasa



Mataji, ya nyumbani na yale ya Ulaya, ninachojivunia ni utamaduni wa vijana walioendeleza kutokana na maono ya  Matt Busby kwa klabu. Wachezaji mahiri kama Ryan Giggs, Paul Scholes na Gary Neville walifanya klabu kuwa na viwango vitakavyodumu daima.
Kumekuwa na wachezaji wanaohitimu toka Manchester United Academy katika kila timu yangu ninayopanga. Vijana wetu wa umri chini ya miaka 21 wameshinda kombe la Barclays chini ya umri wa miaka 21 msimu huu kukiwa na wachezaji nane toka Old Trafford. Ari hii ya kukuza vipaji toka nyumbani itazaa matunda siku moja.
Darasa la 92: Ferguson akiwa Manchester United ameendelea kukuza vipaji kupitia Academy yake.



Kuna vijana wenye vipaji katika nchi hii na kama wakipewa mafunzo sahihi, Ligi yote ya Uingereza itafaidi matunda ya kazi hiyo njema inayofanywa na klabu.
Nimefurajia msimu wangu wa mwisho, si kwasababu tumeshinda Ubingwa wa Uingereza kwa mara ya kumi na tatu. Lakini haikuwa bahati kuutwaa ubingwa. Tulikuwa na haki: wachezaji wadogo waliopata mafunzo, timu imara yenye viwango ambayo haikuwa tayari kushindwa – tulikuwa nyuma kwa jumla ya point 29 msimu huu.






Umati wa watu mkubwa sana. Niliagwa vizuri sana kwenye msimu wangu wa mwisho, lakini mechi yangu ya mwisho katika Old Trafford ni jambo ambalo Mimi na familia yangu hatutasahau kamwe.
Premier League ni ligi inayotambulika kwa jinsi ilivyo maarufu na kuwa na mashabiki wengi. 
Si Old Trafford  tu– pia safari za Goodison, St. James’, Anfield na White Hart Lane zilikuwa miongoni wa ziara zilizotoa ushirikiano. Ni historia na utamaduni wa mchezo wa Uingereza vilivyoleta mafanikio. Nitakumbuka haya yote daima. Lakini nitafurahia kutazama Barclays Premier League kuwa na misimu mingine mizuri, yenye kuvutia na kutoa wachezaji wenye ubora.

Ferguson na Familia yake hawatosahau kamwe jinsi alivyoagwa siku ya mechi yake ya mwisho


0 comments:

Chapisha Maoni