The reliable source of sport news

Jumanne, Agosti 13, 2013

Azam FC Mdebwedo: Yamaliza ziara Afrika ya Kusini kwa kichapo

13.8.13 By Unknown 2 comments

Azam FC imehitimisha ziara yake Afrika Kusini kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji, Moroka Swallows katika pambano lililopigwa kwenye Uwanja wa Volkswagen Dobsonville.
Mchezo dhidi ya Moroka ulikuwa wa tatu kwa kikosi cha Azam, baada ya kucharazwa mabao 3-0 na Kaizer Chiefs, kisha kudunguliwa mabao 2-1 na Orlando Pirates na ushindi pekee wa bao 1-0 dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Katika pambano la jana, bao pekee la Moroka lilitundikwa kimiani na Felix Obada aliyetokea pembeni na kufumua shuti akiwa nje ya 18. Naye kocha Stewalt Hall wa Azam alisema timu yake ilicheza vizuri, lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizopata.

2 comments:

  1. Wamefulia hao, na Yanga tutawapiga nyingi sana tu.

    JibuFuta
  2. Azam timu bora, inahitaji muda tu kwa poa. Italeta changanoto tu, kushindwa mechi hizo chache za kirafiki si kushindwa kila kitu

    JibuFuta