Azam FC imehitimisha ziara yake Afrika Kusini kwa kipigo cha bao
1-0 kutoka kwa wenyeji, Moroka Swallows katika pambano lililopigwa
kwenye Uwanja wa Volkswagen Dobsonville.
Mchezo dhidi ya Moroka ulikuwa wa tatu kwa kikosi
cha Azam, baada ya kucharazwa mabao 3-0 na Kaizer Chiefs, kisha
kudunguliwa mabao 2-1 na Orlando Pirates na ushindi pekee wa bao 1-0
dhidi ya Mamelodi Sundowns.
Katika pambano la jana, bao pekee la Moroka
lilitundikwa kimiani na Felix Obada aliyetokea pembeni na kufumua shuti
akiwa nje ya 18. Naye kocha Stewalt Hall wa Azam alisema timu yake
ilicheza vizuri, lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizopata.




Wamefulia hao, na Yanga tutawapiga nyingi sana tu.
JibuFutaAzam timu bora, inahitaji muda tu kwa poa. Italeta changanoto tu, kushindwa mechi hizo chache za kirafiki si kushindwa kila kitu
JibuFuta