Ukurasa
wa mbele wa gazeti la Madrid, AS kwa mara nyingine limeandika habari za Gareth
Bale leo Alhamisi kuwa kuna maendeleo yaliyofanyika katika mchakato wa uhamisho
wa nyota wa Tottenham Hotspur, Gareth Bale.
Kwa
mujibu wa Marco Ruiz, mwanahabari aliyekuwa akimfuatilia Gareth Bale akiwa
kwenye timu ya Taifa ya Wales, amedai kuwa mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy
yuko karibu kuikubali ofa ya Euro milioni 110 pamoja na beki wa kushoto wa Real
Madrid Fabio Coentrao.
Spurs
awali ilikuwa akimuhitaji Jese Rodriguez au Alvaro Morata kujumuishwa kwenye
dili hilo pamoja na fedha, lakini Real Madrid itamtoa Coentrao wanayempa
thamani ya Euro milioni 30.
Levy
anahitaji Euro milioni 90 pamoja na Coentrao, Real Madrid inaamini kuwa Euro
milioni 85 pamoja na mchezaji huyo wa zamani wa Benfica inatosha.
Tottenham
wanaonekana kutokuwa na haraka kukamilisha mchakato huo, wakati Real Madrid
inajitahidi kukamilisha swala hili mapema iwezekanavyo kabla msimu haujaanza.
“Chanzo
kimoja” kimenukuliwa na AS: ”Bale ameshikilia msimamo wake kwa wiki tatu
sasa. Hataki kufanya mazoezi wala kucheza mechi yoyote… inaonekana amedhamiria
kweli.”
Mwishoni,
AS linaongeza kuwa Spurs haijakata tama kumshikilia Bale na bado wanafikiria
kufanya mazungumzo kwa ajili ya mkataba mwingine na raia huyo wa Wale siku za
usoni.
Kava ya mbele ya gazeti la AS hii hapa.





0 comments:
Chapisha Maoni