"Ikumbukwe
kuwa hivi karibuni , uongozi wa Yanga uliitisha mkutano Mkuu wa dharura
uliokuwa ufanyike tarehe 18 Agost 2013 viwanja vya sabasaba kwenye
ukumbi wa PTA Saa 3:30 Asubuhi kwa lengo la kujadiliana na suala la Azam
Television kurusha mechi za Yanga. Mkutano huo kwa sasa umeahirishwa
kutokana na sababu ifuatayo.
![]() |
| Makamu
Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga kulia akiwa na Mjumbe wa Kamati
ya Utendaji, Abdallah AHmed Bin Kleb kushoto na Kombe la ubingwa wa Ligi
Kuu |
Tarehe
14.8.2014 Naibu Waziri wa Habari, Utamadun,Vijanai na Michezo
Mheshimiwa Amosi Makala aliitisha kikao cha pamoja ,kilichojumuisha
pande zote husika wakimwemo wasaidizi wake, shirikisho la mpira wa
miguu Tanzania(TFF),Mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi ya vodacom , uongozi
wa Yanga sc na uongozi wa Azam Media.
Baada ya kikao hicho yafuatayo ni makubaliano yaliyofikiwa
(a)Klabu
ya Yanga itapata fursa ya kushiriki na kupitia katika utengenezaji wa
mkataba wa udhamini wa haki za matangazo na televisheni wa Azam Media
ili kujiridhisha na vipengele vyote vya mikataba kwamba kwa namna yoyote
haviathiri klabu ya Yanga kufuatia uhusiano uliopo wa Azam Media
wanaotarajiwa kupewa haki hizo na Timu ya Mpira Azam FC moja ya timu
pinzani ya Yanga kwenye ligi ya Vodacom
(b)Kuwepo
na utayari kwa uongozi wa Azam Media kukutana na uongozi wa Yanga
kuzungumzia mahusiano ya kibiashara yatakayo nufaisha pande zote mbili.
Hivyo
basi baada ya kuzingatia hayo uongozi unapenda kutoa taarifa kwa
wanachama wake kuwa mkutano uliopangwa kufanyika tarehe 18 Agosti 2013,
viwanja vya sabasaba kwenye ukumbi wa PTA Saa 3:30 asubuhi umeahirishwa
hadi mtakapotangaziwa vinginevyo, lengo ni kutoa nafasi na fursa kwa
uongozi kufanyia kazi hayo yaliyotajwa hapo juu
Pia
uongozi unawashukuru wanachama na wapenzi wote wa Yanga kwa kuonyesha
ukomavu na kusimamia maendeleo ya klabu yetu kwa Hali na mali, na
uongozi Utaendelea kusimama IMARA katika kuijenga Yanga Mpya
Uongozi
pia unawataka wapenzi wote kuja kwa wingi uwanjani kuishangilia timu
yetu wakati wa mechi ya kugombea ngao ya hisani kuashiria ufunguzi wa
michuano ya kutetea ubingwa tunaoushikiria wa Ligi Kuu ya vodacom,"
Clement Sanga
Makamu Mwenyekiti
Young Africans Sports Club
16.08.2013.




0 comments:
Chapisha Maoni