KOCHA wa Barcelona, Tata Martino
amepuuza taarifa za mpango wa kuwasajili David Luiz au Daniel Agger, kwa
kuthibitisha anafuarahia safu ya sasa ya ulinzi.
Vigogo hao wa Katalunya wamekuwa
wakihusishwa kutaka kuwasajili kwa fedha nyingi wachezaji hao wa klabu
za Ligi Kuu England, Chelsea na Liverpool.
Na kocha huyo mpya amesema katika
Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake wa kwanza wa La Liga
dhidi ya Levante: "Tuna Puyol, Pique, Mascherano, Bartra, pia Adriano.
Ikiwa kuna majeruhi yeyote, usajili wa Januari utakuja miezi michache
ijayo,".
VIDEO Kaangalia Martino
akirithi mikoba ya Vilanova Barcelona

Hahitajiki: Barcelona ilifikiriwa kutaka
kusajili beki wa kati majira haya ya joto na David Luiz (juu) na Daniel
Agger walitajwa kuwamo kwenye orodha ya wanaotakiwa

Klabu hiyo ya Hispania ilisumbuliwa na
tatizo la majeruhi msimu uliopita, iliyowaponza kuchapwa 7-0 katika Nusu
Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich.
Lakini kauli ya kocha mpya inamaanisha
makocha wenzake, Brendan Rodgers na Jose Mourinho wanaweza kutuliza
presha zao.
Rodgers amempa Agger Unahodha Msaidizi
katika kumshawishi abaki Anfield, wakati Mourinho alisema kuhusu Luiz:
"Tunataka kumbakiza na tunafahamu kwamba klabu kubwa kama Barcelona
wanataka kilicho bora na wanajaribu kupata moja kati ya mabeki bora wa
kati duniani, lakini tumekuwa wazi sana kwa kusema kwamba hakuna nafasi
ya David Luiz kuondoka,".

Mambo hadharani: Tata Martino
akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake wa kwanza wa
mashindano tangu aanze kazi Barca




0 comments:
Chapisha Maoni