The reliable source of sport news

Alhamisi, Septemba 19, 2013

ARSENE WENGER: Hatuogopi chochote kwenye michuano ya UEFA

19.9.13 By Unknown No comments

Kocha wa Arsenal iliyojichukulia point tatu za muhimu jana dhidi ya Marseille
Arsene Wenger amedai Arsenal haiogopi chochote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya “Champions League” baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Marseille katika kundi F.
Napoli nayo iko kileleni mwa kundi F ikiwa imefungana point sawa na Arsenal na magoli pia baada ya kuizika Borussia Dortmund 2-1 katika uwanja wa San Paolo.
Arsenal imepata ushindi huo baada ya Theo Walcott kuifungia bao la kwanza na Aaron Ramsey kuweka bao la pili kimiani.

Wenger alisema: ‘Mara zote tunajitahidi kushinda, na imekuwa hivyo.
'Tumecheza mechi nyingi ugenini tukiwa katika hali ya changamoto ya kufungwa.
'Lakini jambo la kufurahisha ni uwezo tulioonyesha, nilijua ni muhimu sana kutumia nafasi hii kujinyakulia point tatu.
'Jana nilisema tunahitaji point 10, nadhani point tatu sasa ni mwanzo mzuri.
'Nilidhani ungekuwa mchezo mgumu kwasababu hata Marseille walikuwa wamejiandaa vema.
Theo Walcott akishangilia bao lake dhidi ya Marseille katika ushindi wa 2-1

Mesut Ozil alionyesha kiwango kizuri kwa mara nyingine tena
'Wanajua wao si chochote na hawana cha kupoteza. Na wafaransa ni hatari sana wakiwa katika hali hiyo.
'Marseille walianza vema kipindi cha kwanza lakini hatukufanya makosa kwenye safu ya ulinzi.
'Nilihisi tusingefanya chochote kwa jinsi nilivyoona mchezo kipindi cha kwanza, Marseille walikuwa wakikimbiza sana na wakimiliki mpira muda mwingi. Walipoa kipindi cha pili na tuliamua kuitumia nafasi hiyo vizuri.'
Aaron Ramsey alifanikiwa kufunga goli lake la sita la msimu huu na kuiwezesha Arsenal kupata bao la pili
Ramsey, ambaye alionyesha kiwango kikubwa alisema: 'Tuliwahi kucheza hapa tukashinda-  Nimefunga pia, tumefanya kama ilivyo desturi yetu na tumepata ushindi muhimu. Ni jambo la kujivunia.

'Nafurahia jinsi ninavyocheza kwa sasa, Nacheza kwa kujiamini na kwa namna nzuri ya kuwakabili mashabiki.

0 comments:

Chapisha Maoni