KLABU ya Barcelona inamtaka kipa wa
Chelsea, Thibaut Courtois awe kipa wao namba moja msimu ujao na imeanza
harakati za kumchukua.
BIN ZUBEIRY inafahamu wamemuweka
juu ya kipa wa Borussia Moenchengladbach, anayepewa thamani kubwa
Marc-Andre ter Stegen katika orodha ya makipa wanaotaka warithi mikoba
ya Victor Valdes.
Huku Petr Cech akiwa hajaonyesha dalili
za kuachia mikoba ya kipa namba moja Stamford Bridge, Mbelgiji huyo
anaidakia kwa mkopo Atletico Madrid keeper na inafahamika anapenda
kujiunga na vigogo wa Katalunya katika kusaka namba ya kudumu kikosi cha
kwanza.



Wakongwe: Lakini ikiwa Petr Cech (kulia)
atabakia Chelsea, Courtois ataombwa kuchukua nafasi ya Victor Valdes
Gharama bado hazijawekwa wazi. Wakati
thamani ya Ter Stegen ni kiasi cha Pauni Milioni 10, Chelsea inatarajiwa
kuomba fedha mara ya tatu ya hizo ili kumuuza Courtois, ambaye amefanya
vizuri katika misimu yake miwili ya awali Madrid.



0 comments:
Chapisha Maoni