Shinji Kagawa alisajiliwa na Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu wa mwaka 2011-12 akitokea Borussia Dortmund. Mjapani huyo alijiunga na timu akiwa kiungo mshambuliaji mwenye kiwango cha aina yake katika ugawaji wa pasi na kuchungulia goli. Pamoja na jitihada zake za msimu uliopita, David Moyes hakuona nafasi ya kumweka katika mchezo Manchester United iliocheza dhidi ya Liverpool. Je, Moyes anaweza kumtumia Kagawa United?
Nafasi gani Kagawa anaimudu zaidi?
Kagawa ametumika zaidi kama kiungo wa kushoto msimu uliopita. Hata hivyo hii si nafasi sahihi kwake, hasa ukizingatia mfumo wa Manchester United wa kutanua na kuleta mpira ndani ya boksi. Kagawa anafanya vizuri akicheza katikati, akicheza kama namba 10, mchezeshaji nyuma ya straika. Kama inavyoonesha picha hapo chini, Kagawa anaweza kutengeneza nafasi zaidi akiwa kati na si kutokea pembeni.Kagawa anatengeneza nafasi sehemu anayostahili kucheza namba 10.Hata hivyo mjapani huyo alifanikiwa kucheza dakika 90 michezo mitano tu msimu uliopita na kufanikiwa kuanza kucheza mechi 17 na kukosa 12. Kwa kiwango cha pasi cha asilimia 90 ni mchezaji mbunifu na mwenye mbinu binafsi anayeweza kucheza kati vizuri lakini amekuwa akitanua kutafuta nafasi badala ya kubaki kati.
Sababu ya yeye kufanya hivi, ni ushindani wa namba Manchester United. Wayne Rooney anacheza vizuri namba 10 pamoja na shutuma za kuwa na kiwango cha chini msimu uliopita lakini alifanya kazi nzuri ya kumlisha Robin Van Persie. Kama Rooney angekuwa ameondoka klabuni, Kagawa angekuwa mchezaji muhimu sana, lakini hili haliwezekani kwa sasa, Kagawa anahaha kupata nafasi dhidi ya Rooney. Danny Welbeck amekuwa akitumika kama mbadala wa Van Persi, jambo linaloonekana kuwa majanga kwa Kagawa.
Mfumo anaoupenda kutumia David Moyes
Kwa hakika, David Moyes amebadili mfumo wa Manchester United kuwa 4-4-2, mfumo usiomfaa Kagawa. Dhidi ya Swansea na Liverpool Moyes alimtumia Danny Welbeck zaidi kama straika wa pili, badala ya namba 10. Kweli kabisa mfumo wa 4-4-2 haumfai Kagawa, mfumo wa straika wa pili ama kama winga. Jambo linalompa Moyes ugumu kupata nafasi ya Kagawa.Dhidi ya Liverpool, Welbeck alijaribu pasi 27, ambacho ni kiwango hafifu sana kwa namba 10, hili linadhihirisha alikuwa kicheza zaidi kwenye eneo la kutafuta goli zaidi, picha hapo chini inaonesha.
Ukilinganisha na Kagawa kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Norwich unaweza kuona tofauti:
Kagawa anatumia muda mwingi katikati, anashuka na kupanda. Pia amegusa mpira mara nyingi ukilinganisha na Welbeck (Mchezo dhidi ya Swansea), kagawa alikuwa na wastani wa pasi 42 kwa mechi msimu uliopita.







0 comments:
Chapisha Maoni