etr Cech is happy for the transfer to go ahead [GETTY]
 |
| Petr Cech anafurahi mchakato wa uhamisho kwenda Barca uendelee |
Miamba ya Hispania wameshaulizia uwezekano wa kumnyakua Peter Cech ili kuirithi nafasi ya Victor Valdes anayetaka kuondoka klabuni hapo.
Cech amefanya mazungumzo na bosi wake Jose Mourinho na inaeleweka kwamba ameshawishika kuondoka ili akapate changamoto mpya baada ya kuitumikia Chelsea miaka tisa akiwa Stamford Bridge.
Ujio wa Mourinho Chelsea umemfanya Cech kuamua kubaki kwa muda. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 31 hafurahii kufanya kazi na Mourinho tena na wawili hao wamefanya mazungumzo ambayo Bosi wa Blues ameonyesha dhamira ya kuleta wachezaji wa kizazi kipya Chelsea.
Mourinho bado anamwamini Cech kama moja ya makipa bora duniani.
Lakini pia ni shabiki mkubwa wa kipa wa akiba wa Chelsea Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 21, ambaye alionyesha kuwa na kiwango kikubwa alipokuwa kwa mkopo Atletico Madrid.
Courtois anatakiwa na timu nyingi na Chelsea imepata ofa nyingi kwa ajili ya Mbelgiji huyo.
Na ana mashaka Courtois hatakuwa tayari kuendelea kusugua benchi tena baada ya kuonyesha kuwa ana kiwango cha kutosha alipokuwa Hispania.
Ripoti zilizotapakaa Hispania zinasema Chelsea na Barcelona zinaweza kuafikiana kubadilishana wachezaji ikiwa ni Cech na Valdes dirisha la usajili litakapofunguliwa January.
Lakini ni wazi Mourinho hana mpango wa kumuacha Cech aondoke ingawa mchezaji anataka kuondoka.
Kipa aliyeitumikia Barca kwa muda mrefu, Victor Valdes anataka kuondoka Nou Camp mwishoni mwa msimu huu.
Wababe hao wa Catalan wameulizia pia uwezekano wa kumsajili Pepe Reina kutoka Liverpool wakati muda wake wa kuitumikia Napoli kwa mkopo utakapokwisha.
“Ilitokea tu. Chelsea walikuja na ofa na kila mtu anajua kwamba nilitaka kuichezea klabu hii tangu nilipokuwa Shakhtar”
Willian
Vyanzo vya karibu na Reina vinadai ameshafanya mkataba wa awali na Barcelona - lakini habari za uwezekano wa kumpata Cech zimewafanya Wahispania hao kupitia upya uamuzi wao huo.
Wakati huo huo, nyota mpya wa Chelsea Willian ameapa kuisaka nafasi kwenye kikosi cha Brazili kupitia English Premier League kupitia Chelsea.
Amesema: “Bila shaka ligi ya Uingereza ni kubwa na inatazamwa na watu wengi. Nadhani hili litaniwezesha kuitwa timu ya Taifa, ingawa itategemeana na kiwango changu pia.
“Ninahitaji kucheza kwa nguvu kuonyesha kwamba nastahili kupewa nafasi. kwanza nataka kuwa na uhakika wa kuanza kwenye kila mechi, Kisha kucheza vizuri ili niitwe [na Brazil], hayo ndiyo malengo yangu.”
Chelsea ilimnyakua Willian toka Shakhtar Donetsk kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 32 aliokuwa anataka kufanya mkataba na Tottenham.
Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema: “Huwa mambo yanatokeaga. Chelsea ilikuja na ofa nono na mimi sikuwa na sababu ya kusita kwasababu kila mtu anajua nilitamani kuichezea klabu hii tangu nilipokuwa Shakhtar.
“Ilinishtua, lakini sikufikiri mara mbili. Na kwasababu marais wote wawili ni marafiki, hilo lilirahisisha mambo pia. Mazungumzo yalikuwa marahisi zaidi.
“Wabrazili wenzangu (Chelsea) waliniita, hasa David Luiz, ambaye aliniambia, njoo haraka. Nilitaka kucheza Chelsea, hata ikiwa na Jose Mourinho, ambaye anafanya vema katika kila alifanyalo.
“Nilipokuwa na mapumziko, nilikuja kuangalia mechi za klabu, kwahiyo ninafuraha kukamilisha uhamisho huu.”
Manuel Pasqual (kushoto) wa Italy na Petr Cech wa Czech Republic wakipambana kwenye mechi za kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia zitakazopigwa Brazili mwaka 2014.
0 comments:
Chapisha Maoni