The reliable source of sport news

Jumatano, Septemba 11, 2013

SHINJI KAGAWA NJE MANCHESTER UNITED, AMUULIZA MOYES KWANINI HAJAMPA NAFASI

11.9.13 By Unknown No comments

Shinji Kagawa
Shinji Kagawa ameripotiwa akiuliza kwanini hana nafasi kwenye mipango ya meneja mpya wa Manchester United, Davis Moyes.
Please ask David Moyes why I’m not in the side,” Kagawa alikiambia AFP baada ya kusawazisha na kuipa Japani nguvu mpya uwanjani dhidi ya Ghana mjini Yokohama.  ”Inakera kutopewa fursa ya kucheza, lakini goli kama lile nililofunga linanipa nguvu ya kujiamini. Natumaini naweza kufanya hivyo kwenye klabu yangu na kuimarisha kipaji changu pia.” [...] ”Ni ngumu kuvumilia kutocheza mara zote. Siku nyingine inakera zaidi — iko kama mawimbi yanakuja na kwenda kuongezeka na kupungua,”

Shinji Kagawa hajatokea kwenye mechi yoyote na Manchester United msimu huu ambapo upande huo wa Moyes una point 4 kati ya mechi 3. Kagawa amehusishwa na kurudi Borussia Dortmund inayoshiriki ligi ya Ujerumani Bundesliga; hata hivyo, dirisa la uhamisho lilifungwa Mjapani huyo akiwa klabuni. Kufuatia usajili wa siku ya mwisho wa Marouane Fellaini, wengi wamejiuliza maswali kama nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 anayo nafasi Old Trafford.
Je kuna haja ya Manchester United kumruhusu Kagawa kuondoka? Je Moyes anaweza kumpa nafasi?

0 comments:

Chapisha Maoni