The reliable source of sport news

Alhamisi, Septemba 19, 2013

MNYAMA AMEAMKA RASMI: Simba yaifanyia kitu mbaya Mgambo JKT yaicharaza kipigo cha mabao 6-0

19.9.13 By Unknown No comments

Mshambuliaji wa Simba SC, Amisi Tambwe kulia akipiga shuti mbele ya 
mabeki wa Mgambo JKT katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom 
Tanzania Bara jana
Mnyama Simba ameamka, leo amefanya mauaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar baada ya kuishindilia Mgambo kwa mabao 6-0.

Mrundi Amis Tambwe ameibuka na kufunga mabao manne huku mengine yakifungwa na Haruna Chanongo na beki wa Mgambo akajifunga moja.

Mgambo walionekana kuuanza mchezo kwa kasi lakini wakazidiwa na kasi ya Simba ambayo ilikwenda mapumziko ikiwa na mabao manne.
Katika mechi iliyopita, Simba iliifunga Mtibwa Sugar kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja huo.
Mashabiki wa Simba walikuwa wanashangilia kwa nguvu muda wote huku wakiwadhihaki Yanga ambao timu yao ilitoa sare ya pili mfululizo mjini Mbeya dhidi ya Prisons.

Pamoja na kushinda, Simba ilicheza kwa kasi kubwa huku wachezaji wake wakionyesha kujiamini na kuwapa wakati mgumu wageni wao.

Sasa Simba imefikisha pointi 10 na kukaa kileleni baada ya kushinda mechi tatu na kutoa sare moja.
Betram Mombeki wa Simba akichuana na beki wa
Mgambo JKT, Katika ushindi wa 6-0.

0 comments:

Chapisha Maoni