The reliable source of sport news

Alhamisi, Septemba 19, 2013

Messi apiga Hat-trick Barca ikishinda 4-0 dhidi ya Ajax, amebakisha magoli 9 kuvunja rekodi ya Raul Gonzalez ya mabao 71

19.9.13 By Unknown No comments

Lionel Messi akisherehekea bao lake la kwanza akiwa na Dani Alves kwenye mechi dhidi ya Ajax Septemba 18, 2013
Lionel Messi alifunga hat trick wakati Barcelona ilipokuwa inafungua pazia la michuano ya Klabu bingwa Ulaya (UEFA Champions League) kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ajax jana Jumatano.

Ilikuwa ni habari tofauti kwa Jose Mourinho ambaye Chelsea ilishindwa kufurukuta mbele ya FC Basel ya Uswais baada ya kupewa kipigo cha mabao 2-1 ikiwa Darajani huku bao pekee la Chelsea likiwekwa kimiani na Oscar.

Washindi wa pili wa michuano hiyo ya UEFA wa msimu uliopita, Borussia Dortmund nao walijikuta wakianza michuano hiyo vibaya kwa kuchezea vitasa toka kwa Napoli baada ya kufungwa mabao 2-1 na kocha Juergen Klopp na kipa Roman Weidenfeller wakizawadiwa kadi nyekundu kila mmoja.

Katika uwanja wa Nou Camp, Lionel Messi alifanikiwa kufunga magoli yake katika dakika ya 22, 55 na 75 wakati Gerard Pique akifunga bao la nne dakika ya 69.

"Barcelona imesheheni vipaji," Kocha wa Barcelona alisema. "Leo tunaweza kuwazungumzia Messi na Valdes, siku nyingine tutawaongelea Xavi au Neymar. Ni kawaida mmojawapo anapong’ara kwa wakati fulani."

Magoli matatu ya Messi yanamfanya apungukiwe na mabao tisa tu kuweza kuvunja rekodi ya Raul Gonzalez ya mabao 71 kuwa mfungaji wa muda wote wa UEFA.

Barcelona na Milan zinaongoza kundi H.
Fursa Iliyopotea: Kolbeinn Sigthorsson wa Ajax akipiga penati iliyoishia mikononi mwa Victor Valdes

0 comments:

Chapisha Maoni