Manchester:
Meneja wa Manchester United David Moyes amekiri kuwa na mpango wa kuongea na Winga wa England Ashley Young kufuatia tabia yake ya kujiangusha iliyoleta utata Man U iliposhinda 2-0 dhidi ya Crystal Palace jana Jumamosi.
Young amekuwa gumzo kwanye ushindi wa kwanza wa David Moyes akiwa Old Trafford Jumamosi baada ya Young kutafuta penati kwa nguvu kwa kiujiangusha alipokabwa na Dikgacoi.
Kiungo wa Dikgacoi alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja lakini wageni hao wa Old Trafford hawakurudisha nyuma majeshi, Young naye aliingizwa kwenye kitabu cha mwamuzi kwa tabia mbaya ya kujiangusha alipogongana na kiungo huyo.
Meneja wa Manchester United David Moyes amekiri kuwa na mpango wa kuongea na Winga wa England Ashley Young kufuatia tabia yake ya kujiangusha iliyoleta utata Man U iliposhinda 2-0 dhidi ya Crystal Palace jana Jumamosi.Young amekuwa gumzo kwanye ushindi wa kwanza wa David Moyes akiwa Old Trafford Jumamosi baada ya Young kutafuta penati kwa nguvu kwa kiujiangusha alipokabwa na Dikgacoi.
Kiungo wa Dikgacoi alionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja lakini wageni hao wa Old Trafford hawakurudisha nyuma majeshi, Young naye aliingizwa kwenye kitabu cha mwamuzi kwa tabia mbaya ya kujiangusha alipogongana na kiungo huyo.
Young alionywa na Meneja aliyepita wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kuiacha tabia hiyo ya kujiangusha misimu miwili iliyopita, meneja mpya pia ameeleza hawezi kuvumilia tabia hiyo.
"Mara zote nimesema sipendi tabia ya kujiangusha. Alikuwa na haki ya kuadhibiwa" Alisema Moyes. "Sipendi wachezaji wangu wajiangushe makusudi, sitaki yeyote afanye hivyo."
"Kwa hakika namwambia Ashley hicho kitu sikipendi."
Moyes alifurahishwa na penati, alidai kuwa penati ilikuwa halali na mwamuzi alifanya maamuzi sahihi, penati hiyo ilipigwa na Robin van Persie.
"Wakati mwingine maamuzi magumu yanapaswa kufanyika," alisema Moyes.
"Aliwasiliana na mshika kibendera, maamuzi ya penati yakafanyika, kiukweli tulistahili kwasababu tumejaribu kusumbua golini kwao mara nyingi."
Goli la pili la United lilitoka kwa Wayne Rooney, aliyeingia uwanjani akiwa na kidonda kilichofunikwa kichwani."Vilevile tumefanya uamuzi mgumu kumchezesha Rooney ambaye hajapona vizuri," Moyes added.
"Tulitaka kujua hali yake inaendeleaje, tulipokutana naye, alisema yuko sawa na anaweza kushuka dimbani na angeweza kuvaa bandeji kichwani.
"Sijui ni aina gani ya bandeji aliyovaa kichwani lakini haikuwa maalumu hata hivyo, nadhani ni kama sumo wanazovaa wacheza miereka.
"Hakukuwa na shida yoyote, alionekana kutokuwa na wasiwasi na nilimwona akipiga mpira kichwa mara kadhaa.



0 comments:
Chapisha Maoni